Rais Magufuli aivunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Magufuli ameivunja Halmashauri hiyo na kuipandisha hadhi Halmashauri ya Manispaa ya Ilala kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuanzia leo Februari 24, 2021

Ameipandisha hadhi Halmashauri hiyo kwa Mamlaka aliyonayo chini ya Kifungu cha 5(1) cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Sura ya 288

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Waziri wa Nchi - TAMISEMI, taratibu nyingine za kisheria ikiwemo kuhamisha shughuli za Halmashauri ya Jiji ya Dar iliyovunjwa zinakamilishwa

B12AFB56-E91D-45FF-AA43-E7DB46471C8A.jpeg

F5E6A22E-A016-483C-9E98-F9E63606F2B2.jpeg
4B15F5A1-AE35-4FE5-B493-DBA6306A44F4.jpeg
72D54F27-854B-40D4-AF8C-AEEE124B65FB.jpeg
C8589832-3334-4F8E-9C15-91B2099429A5.jpeg
724A0E68-80F9-4EA2-8DB5-F4D62C10F2B4.jpeg
10202046-5DE9-4CE0-BA0B-FA49D4673DF3.jpeg
 
Tatizo la Jiwe no kupenda attention...na hii ndiyo Kiki aliyoipanga kuja nayo baada ya kutumbua kuishiwa nguvu

Dar itabaki kuwa jiji hata akiifanyia figisu....na Chato kitabaki kuwa kijijini. Kamwe hawezi kugawa jiji la Dar vipande vipande.

Unapozungumzia Jiji la Dar es Salaam unazungumzia manispaa za Ilala,Temeke,Kigamboni,Kinondoni na Ubungo. Hizo ni mbwembwe na kutaka attention! Kwa maana nyingine Dar ea salaam itaendelea kuwa na hadhi ya Jiji regardless mgawanyo wa kimamlaka wa kiserikali za mitaa

Kiutawala itasomeka hivyo na kuleta ukakasi manispaa ya ilala kuitwa Jiji la Dar es salaam.

Kiutendaji halmashauri ya Jiji (DCC) iliyovunjwa haikuwa na kazi! Kwa kuwa manispaa zilikuwa zinajitegemea na zilikuwa na nguvu ya kufanya maamuzi ya bajeti zake za ndani. Rais alitakiwa avunje Mamlaka iliyoitwa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam (Dar city council). Hili ndio aliopaswa ashauriwe.

Halmashauri ya Jiji ni ngazi ya juu kabisa katika Mamlaka za serikali za mitaa ikifuatiwa na Manispaa,(Municipal Councils), halmashauri za miji (Town Councils) na halmashauri za wilaya (District councils). Mgawanyo huu unaathiriwa kwa kiwango kikubwa na uwezo kimapato,uwepo wa shughuli za Kiuchumi k.v viwanda,uwepo wa huduma za Kijamii k.v vyuo n.k

Dar es salaam hakuna wilaya inayoitwa D'salaam kama ilivyo Dodoma,Tanga au Mbeya hivyo haileti maana Ilala kuwa halmashauri ya Jiji la Dar es salaam, ni sawa na kuipa jina Wilaya ya Ilala kuwa na jina jipya wilaya ya Dar es salaam. Hapo ndipo utapata Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam
 
Korona ipo na inaua, vaa barakoa nawa mikono maji safi pia usisahau kukaa mbali na mikusanyiko isiyo na ulazima.

NB: Waziri kapata nafuu na Maalim Seifu hatuko nae duniani.
Usiogope Dr Tulia aliugua mara mbili lakini anadunda kama kawa!

MwanaFA aliugua na sasa yuko bungeni

Piere Liquid aliugua na sasa ni meneja wa Saidia Simba Ishinde

Usiogope bwashee chukua tahadhari
 
DSM ilikuwa inaundwa na manispaa nne kinondoni, Ilala, Ubungo na Kigamboni

Halmashauri ya jiji la DSM ilikuwa inasimamia halmashauri za manispaa zote nne lkn haina eneo lake rasmi la kiutawala, halmashauri ilikuwa na uwezo kuuchukua mradi wowote katika manispaa yyte na kuendeleza na kugawana manispaa inayopatikana mradi kwa utaratibu maalum, hvyo alichokifanya ni sahihi tu.
Naomba msaada wa kueleweshwa hapa wakuu, hii ina maana gani na itakuwa na tofauti gani na ilivyokuwa mwanzo, pia faida zake hasa kwa sisi tunaoishi kwenye hilo Jiji linaloitwa Ilala kwa Sasa?
 
Back
Top Bottom