Rais Magufuli aipa Wizara ya Ujenzi na Tanroads wiki moja kutia saini makubaliano ya mkataba wa ujenzi wa daraja la Kigongo-Busisi

Kwa busisi daraja hilo litakuwa kiungo kwa usafrishaji kwenda maeneo kongo uganda burundi na rwanda
 
Daraja la kigamboni limeunganisha wilaya tatu?
Wilaya mbili Dar ni raia milioni mbili ongezea na Udogo wa Dar(Dar inaingia mara tano ili kufikia ukubwa wa wilaya moja), na Dar ndio hub ya biashara hapa TZ, ipo bandari pale pia lipo soko la Africa mashariki la Kariakoo etc
 
At least ungesema hospitali, mavyuo tunayo mengi, labda kuyaboresha tu. Hospital ni tatizo sana maeneo mengi Nchini.
Of course mkuu, mi nilikuwa nimechomekea tu

Tusisahau kuinvest for the future, Nigeria wanalia huko vyuo vya serikali ukijumlisha na vya Private udahili unapwaya maana wanaostahili kwenda vyuo huko Nigeria ni wengi sababu hawakujenga vyuo vya kutosha kipindi cha nyuma
 
Naona hujawahi kupita hapo

Kwa taarifa yako ndio kiungo mhimu cha ukanda wa ziwa na mwanza ambayo ndio centre zone

Magari yote ya mwanza to Geita, Bukoba Kampala zote zinapita hapo

Fanya utembelee hata mara moja uone ambulance zinavyopanga foleni zikiwa na wagonjwa ndani labda utaona umhimu wake

Hilo daraja ni mhimu kuliko hata daraja la nyerere kigamboni
Kweli mkuu
 
Dah

Aisee hiyo pesa inaweza jenga vyuo vikuu saba vikubwa kabisa halafu inatumika kuunganisha wilaya mbili !

Jamani kwanini tumekuwa hivyo ujenzi wa daraja ni muhimu sana, watu wana shida Sana kule, kama ukipata muda tembea uone, kutumia busara kabisa wana haki kupata daraja, Mambo ya ujenzi wa vyuo awamu itakayofwata, kakwambia watu wanakufa asubiri kujenga vyuo
 
Quote "Abdallah Atiki alisema vivuko vya Mv Mwanza na Mv Misungwi husafirisha kati ya abiria 6,500 hadi 8,000 na magari 730 kwa siku." Unquote

Jee Daraja litakalo gharimu Billion 700, ni stahiki kujengwa kama wasafiri kwa siku ni 8000 na magari 730?

Ndio maana wafadhili wamegoma kuufadhil mradi huu. Mheshimiwa Raisi analazimisha mambo bila kuangalia faida na hasara
 
Quote "Abdallah Atiki alisema vivuko vya Mv Mwanza na Mv Misungwi husafirisha kati ya abiria 6,500 hadi 8,000 na magari 730 kwa siku." Unquote

Jee Daraja litakalo gharimu Billion 700, ni stahiki kujengwa kama wasafiri kwa siku ni 8000 na magari 730?

Ndio maana wafadhili wamegoma kuufadhil mradi huu. Mheshimiwa Raisi analazimisha mambo bila kuangalia faida na hasara
We sema la gharama gani linastahili kujengwa hapo maana bil700 inaonekana ndo hoja yako kwa namna ulivyoisuka sentensi yako.
 
Naona hujawahi kupita hapo

Kwa taarifa yako ndio kiungo mhimu cha ukanda wa ziwa na mwanza ambayo ndio centre zone

Magari yote ya mwanza to Geita, Bukoba Kampala zote zinapita hapo

Fanya utembelee hata mara moja uone ambulance zinavyopanga foleni zikiwa na wagonjwa ndani labda utaona umhimu wake

Hilo daraja ni mhimu kuliko hata daraja la nyerere kigamboni
Ni jambo jema lakini wagonjwa hawafanyi hilo liwe muhimu. Kwani ikijengwa hosp huo upande wenye shida huoni itasaidia kuokoa hayo maisha badala ya hizo safari tena za gari.
 
Kama kuna mazuri aungwe mkono.. Lakin awakumbuke KASKAZINI KIDOGO pale Mto wami.. AWEKE DARAJA LA KISASA KUOKOA MAISHA YA WATU WENGI WANAOPATA ULEMAVU..
SISI NI WAPUMBAVU SANA. ILI NCHI IWE SAWA LAZIMA VITU VIFANYIKE KWA STRATEGIC PLAN, hivyo hilo daraja angalau lina mashiko kuliko lile la coco..
 
Ni muhimu sana hilo daraja na hasa kiunganishi kati ya mkoa wa Mwanza na mikoa ya Kagera & Geita +Uganda +Maziwa Makuu.Tatizo kubwa hapo ni kwamba hivyo vivuko siyo reliable sana kuna wakati kinakuwa kimoja na magari ni mengi sana unaweza kusubiri hadi dakika Zaidi ya 60 (kama una gari) ukisubiri kuvuka.Kuvuka ng'ambo moja hadi nyingine ni dk 30 hivi.Kuna issues kadhaa hapo za kiuchumi e.g
(a)Mkoa wa Geita unaongoza kwa uzalishaji wa dhahabu nchini kwa migodi mikubwa,ya kati na midogo,kuna movements sana za Geita-Mwanza-Geita.Serikali inataka Sekta ya madini ichangie 10% kwenye GDP badala ya 4.2% ya sasa,nk,nk...
(b)Ni barabara kuu ya Mwanza-Kigali,Bujumbura,Congo DR (Mashariki) wafanyabiashara wanapeleka samaki maarufu kama mapanki huko,nk!.Kuna Kampala-Mwanza Pia unaweza kutoka eneo la maziwa makuu ukapita mwanza hadi Kisumu huko nk.
(c) Mkoa wa Kagera pia unaitegemea hiyo barabara,maji peke yake hayatoshi!!
HOW CAN WE INCREASE MINERAL PRODUCTION THROUGH THAT BRIDGE? Jman tunatoa porojo sana.
Hii maana yake BARABARA YA MTWARA-DAR IMEONGEZA UZALISHAJI WA KOROSHO,, ASEEE ARE WE SERIOUS??
 
Hongera JPM kwa uamuzi,daraja hili ni kiungo muhimu sana kwa ukanda ziwa magharibi.Hata kama watumiaji watalipia litalipa zaidi ya Daraja la Nyerere Kigamboni.
 
Back
Top Bottom