Uchaguzi 2020 Rais Magufuli aingilia kampeni za Tundu Lissu Kazuramimba Kigoma

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,555
35,880
Wakati Tundu Lissu akiwa uwanjani huko Kazuramimba Kigoma amepita Rais Magufuli akasimama barabarani na kufanya mkutano karibu kabisa na alipo Tundu Lissu ambapo ameahidi kutoa milioni 10 siku chache zijazo.

Kwa mujibu wa ratiba ya tume, Magufuli leo hapaswi kuwepo Kigoma kwa ajili ya kampeni.

Maswali yangu:
Rais Magufuli alidhamiria kubaki Kigoma ili kufanya haya?

Kwanini anashindwa kuheshimu demokrasia?

Je, ingekuwa ni Tundu Lissu kamfanyia hivyo nini kingetokea?

Nini dhamira yake?
Tundu Lissu leo Kazuramimba-Uwanjani kwa mujibu wa tume
20200920_154916.jpg


Magufuli Leo Kazuramimba-Makao makuu ya wilaya pembezoni mwa barabara. Mkutano alioandaliwa na CCM
tanzania_ya_kijani_20200920_154256_2.jpg
 
Du! Kama hayo ni kweli, mbona hiyo ni dalili ya kuchanganyikiwa? Halafu shida ya mtu kama Magufuli ambaye katika hali ya kawaida anataka kusifiwa badala ya kushauriwa, mambo yakienda kombo hataweza kusikiliza ushauri. Ni amri kwenda mbele, na atazidi kujichanganya.
 
Serikali dhalimu na Dikteta huwa wanafanya nchi na wao kama serikali na kiongozi kuwa kitu kimoja Eti ukimkosoa dikteta umekosoa nchi Ukipinga sera za serikali, we msaliti wa nchi Kiuhalisia unaweza kupinga serikali, kiongozi na kwa kufanya hivyo ukawa mzalendo.
 
Ndio raha ya kuwa mgombea lakini hapohapo rais wa nchi ,ameonyesha bado ana mamlaka hata kama kwa sasa ni kipindi cha mpito kikatiba( kipindi cha uchaguzi)

Sasa basi anaweza kuwaagiza hata wenye mamlaka ya uchaguzi (tume), vyovyote anavyotaka yeye.

Tunaongea kila siku kwamba huu uchaguzi ni kukamilisha tu ratiba ili kuondoa lawama,Rais ataendelea kuwa Magufuli. Hapo tayari ubabe na dharau vimeshatumika.mjiandaae kisaikolojia tu na matokeo.
 
Kumbuka Magufuli bado ndio rais wa nchi hii, yaani aache kutekeleza mipango ya maendeleo kwa sababu kuna chizi mmoja anayedhani anaweza kuwa rais wa nchi anaongea matusi yake! Hell no!! lazima maisha yaendelee
Kumbuka kuwa nje ya kura, Magufuli ni binadamu kama wewe na mimi, hakuzidi na wala hanizidi chochote. Aheshimu taratibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakati Tundu Lissu akiwa uwanjani huko Kazuramimba Kigoma amepita Rais Magufuli akasimama barabarani na kufanya mkutano karibu kabisa na alipo Tundu Lissu ambapo ameahidi kutoa milioni 10 siku chache zijazo.

Kwa mujibu wa ratiba ya tume, Magufuli leo hapaswi kuwepo Kigoma kwa ajili ya kampeni.
Leo Magufuli ametuthibitishia kuwa vurugu wanazofanyiwa wapinzani zinafanywa law baraka zake na maelekezo anafanya yeye.

Pia Rais Magufuli leo amethibitisha kwamba uchaguzi huu si lolote kwake hata kama atashindwa atang'ang'ania kukaa madarakani kwa nguvu.

Leo pia imethibitisha kuwa Magufuli anataka kubadili katiba ya nchi abaki kuwa rais wa Miller.

Ni wakati sasa wapinzani waache kunadi ilani waanze kunadi mapinduzi ya kumuondoa madarakani kabla hata ya tarehe 28 October.
 
Back
Top Bottom