Rais Magufuli aidha amedanganywa kuhusu Barakoa au kuna tatizo sehemu (kwa alichoongea leo Feb 21, 2021)

Umelallnika bila kua na hoja kama mtu anae jitamhua ama alie soma
Ungekua unajitambua baada ya vihoja vyako ungetoa na suluhisho
 
Kuna kipindi barakoa za mahospitali (surgical mask) ziliadaimika sana hadi mahospitalini kiasi kwamba hadi madaktari walianza kulaumu kwa kukosa kitendea kazi hicho muhimu. Kilichotokea ni kuzuiwa uingizwaji wa barakoa nyingi ambazo zilikuwa si salama. Sasa hivi hilo tatizo limepungua baada ya MSD kuanza uzalishaji wa surgical mask. MSD wameanza uzalishaji mwezi wa tisa mwaka jana. Pia serikali baada kugundua kuwa kuna barakoa nyingi zisizo salama zimeingia nchini walifanya msako kwenye maduka ya mauzo.
Great work, mnafanya kazi nzuri so far.

Lakini, wewe kama mwana JF ambaye upo for almost 11yrs kama active member (na unakumbuka why we exist): Unakubaliana nami kuwa kauli ya Rais leo ina makosa?

Natambua, kwa nafasi uliyo nayo inaweza kuwa ngumu kukiri, ndani ya nafsi unanielewa vema tu.

Tuseme kweli mlifanikiwa kuziondoa hizo masks mtaani, leo alikuwa anaongelea nini? Kuwa we are compromised hadi leo?!
 
Korona isingeingia sebuleni angeendelea kutangaza dawa ya Bupiji. Rais utafikiri Miganga WA kienyeji toka Sumbawanga.
Unajua unaweza kumfananisha rais na mganga wa kienyeji kutoka Sumbawanga, halafu ukawa umemtukana huyo mganga wa kienyeji kutoka Sumbawanga kwa kumfananisha na rais huyu.

Mganga wa kienyeji akakwambia hata mimi na magumashi yangu yote sijafikia magumashi ya Magufuli tafadhali usinifananishe naye unanionea bure.
 
Let’s assume unasema ukweli na sisi tunaoohoji ndo hatujielewi:

1) Mwaka jana (2020) ni NANI alikuwa Rais wa Tanzania? Ilikuwaje Taifa likafanyiwa hujuma hii bila kushtukiwa? Usalama wetu kama Taifa ulikuwa compromised? Nani hasa walizileta? Walichukuliwa hatua gani na umma ulijulishwa?

2) Kama Sept 2020 (unavyodai) zilizalishwa masks za kutosha, kwanini leo aongelee masuala ambayo yamepitwa na wakati? Si hazipo hizo? Kwanini aongelee kisichokuwepo? Na, kwanini wakati wa kampeni alikuwa anadai “Tumeimaliza Corona nchini mwetu” hadi baadhi ya maigizo yakafanywa na kanisa flani kutoa certificate ya ushindi dhidi ya Corona?

Hapa umeamua kusimama hivi, ni haki yako. Lakini, umeelewa nilikuwa namaanisha nini. So, TZ mna mpango wa kuondoa dawa za kemikali au nazo zitaendelea kuwepo sokoni?


Ukiwa Rais, ukiamua KUTAJA mfano dawa au bidhaa - taja zote. Kataja mbili, watamtumia sauti yake na video for marketing. Wrong!

BTW, jifunzeni kukosolewa kwa nia ya kujenga. Yeyote anayewakosoa mnamwangalia kwa jicho la chuki tu. Tunajenga Tanzania moja mkuu!

The approach was totally wrong. Nafasi ya Rais msiichukulie poa, come again. Think about it!

Nashauri: Fikiria nafasi ya Rais kama Mfariji Mkuu wa Taifa, utaelewa. Hapo bado amechemka! He needs to know his limits and his obligations. Bahati mbaya huenda unanisoma ukinifikiria kama nisiyemtakia mema Magufuli!

Hahaha, mkuu nadhani hujui unayeongea naye ni nani. Nalijua Kanisa vema! Simply - change the approach. Iheshimuni madhabahu
Simply sijaona kosa la Magufuli, bali ninachokiona ni chuki binafsi tu. 2020 alikuwa Rais yeye but hii ni vita, na vita ina mbinu nyingi na ndio maana hata vifaa vya kupimia corona walivishtukia baada ya kuona matokeo yanayotoka yana mashaka. Kumbuka wakati wanashtukia vifaa, of which kipindi hicho bado vifaa vya upimaji vilikuwa vichache kupatikana hata huko wanakotengeneza, tayari kulikuwa na kontena nyingi tu za barakoa zimeingia na zikapimwa kama zimefikia viwango vya kawaida bila kujua hizo ni carier za virus. Ishu ya mapapai ndiyo iliyofungua macho na kujua kumbe hata barakoa zina changamoto kama ambavyo baadhi ya vifaa vya upimaji. Nadhani unajua nini kiliwapata watu wa maabara kuu ya serikali ambapo ndani yake kulikuwa na watu wa usalama wa taifa ambao kiutaratibu sisi wananchi haturuhusiwi kisheria kujua wamechukuliwa hatua gani.
 
Shida yenu hampendi kuambiwa ukweli, barakoa ziliingizwa nyingi sana kipindi cha mwaka jana, na baada ya serikali kugundua hilo walianza kuzuia baadhi ya barakoa zinaonekana zina walakini, na ndio maana kuna kipindi surgical mask zilikuwa adimu hadi mahospitalini kiasi kwamba madaktari walianza kulalamika. Ili kukabiliana na changamoto hiyo, MSD walifanya dharura ya kujenga kiwanda cha kuzalisha barakoa za mahospitalini (surgical mask) amabapo kimeanza full production mwezi wa tisa mwaka jana.
Kwahio badala ya kuhakikisha mbovu haziingii unaona ni sawa kutoa taharuki kwamba zinazotoka nje zina matatizo ?, Mteja layman asiye na kipimo kwenye macho atajuaje ipi ndio na ipi sio (au ndio kuwaambia wasivae barakoa yoyote ambayo sio made in Tanzania)

Na je wale walioleta ambazo ni nzuri (TBS wamezipitisha ) nao unasemaje ?, Pia unataka tuamini kwamba viwanda vyetu sasa vipo bora kiasi kwamba quality ni top notch ? Kumbuka ni hivi hivi viwanda watu wakinunua khanga au shati linapauka likipigwa upepo tu let alone ukifua...

Na hawa wazungu ni wajinga kiasi gani waweze kuweka sumu kwenye barakoa tu na sio vitu vingine ambavyo kila siku vinaingia ? Na kama waligundua hilo na evidence wanayo kwamba kampuni fulani ilileta misaada ya barakoa zenye matatizo ni hatua zipi zimechukuliwa ili kuwawajibisha ?
 
Back
Top Bottom