n00b
JF-Expert Member
- Apr 10, 2008
- 1,006
- 2,667
Wakuu,
Nimemsikiliza Rais Magufuli akiwa anaongea leo kanisani. Nimeshtuka, Rais anaongea kama layman kabisa. Hii ni hatari kwa Usalama wa Taifa kwa mtu ambaye amepewa dhamana ya juu kabisa hapa nchini.
Rais ni Comforter-in-Chief hivyo kama mfariji mkuu wa Taifa ana mamlaka makubwa aliyobebeshwa na hili inaelekea Magufuli analisahau sana. Huwezi toka huko na kuanza kuwambia watanzania eti “Kufa tutakufa tu”.
Rais ni kama BABA katika familia, na kwa Taifa yeye anasimama kama kichwa cha familia. Huwezi kuwa baba bora ukawa unatishia watu wako (wanao, mkeo, ndugu n.k). Kama baba, unaweza kulaumiwa, unaweza kuliliwa, unaweza kupongezwa, unaweza kuumizwa na hatutarajii kuwa utaitangazia familia kuwa wakome kufanya hivyo! Utakuwa umeshindwa kutekeleza majukumu yako.
Rais ni KIUNGO katika Taifa. Unapotokea mgawanyiko, ana wajibu wa kuhakikisha Watanzania wanakuwa wamoja. Hili limekuwa likionekana kuwa tofauti kwa Rais wetu huyu.
Rais anapotoa kauli, ni kauli ya Taifa si yake. Mambo mengi anayoongea Magufuli watanzania walio wengi (wanaojielewa) watakubaliana nami kuwa si yale ambayo kimataifa tungependa kiongozi wetu ayaongee kwa niaba yetu!
Msikilize:
Sasa:
1) Magufuli leo kaongea UONGO mwingi kuhusu barakoa. Alichokiongea ni matusi kwa serikali yake mwenyewe!
- Kama barakoa zilizoingizwa nchini zina virusi au hazifai; kwanini watendaji wake wameziacha ziingizwe sokoni? Anataka kutuambia kuwa TBS na TFDA hawajui kazi yao? Kwanini watendaji wakuu wa taasisi hizi bado wapo kazini?
- Tukubali kuwa tumeingiziwa barakoa zenye kuwa na virusi ambazo zitawaua watanzania: Kwanini Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa, IGP na CDF bado wapo kazini? Taifa letu manake usalama wake upo hatarini. Kwa mantiki hiyo, maduka ya madawa yavamiwe mara moja na barakoa zote ziondolewe sokoni
2) Magufuli amekuwa Rais wa kwanza mimi kumuona akiwa anahubiri katika Ibada za Kanisa Katoliki. Huu ni utaratibu wa kawaida kwa wakatoliki? Halafu anawachamba viongozi wa kanisa kwa kuhimiza waumini kujilinda?
3) Rais ametangaza dawa kadhaa kama Bupiji, COVIDOL etc, anataka kuwaaminisha watanzania kuwa Sayansi nyingine haifanyi kazi tena? Kuwa watanzania wasiziamini dawa nyingine zinazotolewa hospitali tena? Haya matangazo ya dawa za asili imekuwaje hadi wasaidizi wake wamwacha hadi ataje baadhi ya dawa moja kwa moja (kwa kutaja baadhi tu)? Ana maslahi nazo? Nasikia mtu aliwahi kuwa RC wa Dar ana mkono kwenye pharmacy chain flani, na kuna tetesi kuwa yupo kwa niaba ya ‘mzee’; hii haoni inazidi kujenga hisia zisizo sahihi?
Nitarejea