Hatukatai anaweza kuzungumza ila hawez kuingilia utaratibu wa kanisa kwasababu kanisa hupokea miongozo kutoka kanisa kuu ambao wanaamini yanatoka mbinguni. Je ni sahihi rais kulipa muongozo kanisa katholic tofauti na papa? Je kwann rais akejeli waumini hadhari kwsababu mamb ya imani kila mtu anaongozwa na Mungu kwa namna yake na hakuna uthibitisho wa macho unaoona nani nd kaongozwa vizuri. Ndyo maan bible inasema usikuhumu usihukumiwe. Yule ajionae mkubwa kuliko wote basi nae ni mdogo kati yao katika ufalme wa mbingu. Je unawezaje kumuambia mtu kuwa huna Imani ndo maan unavaa barakoa wakati huo umeingia na bunduki kanisani? Kumbuka story ya mtoza ushuru na farisayo.Walivyo sema serikali haina dini, ilikuwa kuwa tofauti na kidogo na nchi za Mataifa ya nje ambayo yalitutawala. Kwani yote yaliongozwa kwa mfumo wa dini, si tu dini bali dhehebu. Mfano Sweden, Ujerumani wao walikuwa Waromani baada ya Mageuzi ya Martin Luther watawala wa nchi hizo waliamua nchi zao ziwe za Kirutheri. Nyerere aliposhika madaraka akasema serikali haina dini. Hii ilimaanisha zaidi kutokuwa na kanisa au kutokuwa na imani ya Uislamu itakayo ongoza Taifa. Hii ndo maana ya serikali haina dini. Ila serikali inaamini Mungu yupo na watu wake wanadini.
Rais hajaongelea dini. Ameongelea mambo ya kitaifa kwa ujumla yanayowagusa wananchi wake. Ndo maana hata kanisa au uslamu wanaongelea mambo ya jamii. Mfano makanisa kadhaa yametoa waraka juu ya tahadhari za Covid 19. Uwezi tenganisha policy na kanisa. Serikali inakataza kutenda maovu, pia dini inakataza kutenda maovu. Ndini ipo kuboresha au kujenga imani ya mtu kwa Mungu wake lakini ipo pia kujenga maisha ya kijamii na huduma mbalimbali. Ndo maana dini au madhehebu yanatoa huduma za kijamii ambazo utolewa na serikali. Nenda kokote duniani uwezi tenganisha. Dini uwafunza watu maisha ya ujasiriamali, afya, elimu, na mazingira haya yote ufanywa chini ya sera za serikali.
Rais alichoongelea ni tahadhari ya kiafya kwa ujumla, hakubagua wala kuonesha maswala ya kidini. Rais ni wa wote, anapo pata nafasi ataongelea maswala ya kitaifa. Si rais wa kwanza kuhudhuria ibada. Marais wengi ufanya hivyo na ndiyo maana wakati wa sherehe za Idd kwa waislamu ualika viongozi wa kitaifa awe Rais, Makamu, hata Waziri Mkuu kuhutubia. Ili limekuwepo toka uhuru na uwa haijarishi Rais ni Mwislamu au lah! Kipindi hicho Rais uweza kutoa sadaka kwa vituo mbalimbali vya watoto yatima mfano Mbuzi, mafuta ya kula, sukari na kadharika. Kwa wakristo pia wakati wa Krismas au Pasaka ualika viongozi wa kitaifa. Limekuwepo miaka yote.
Tuache chuki, hata kama tutaweka chuki yeye tayari ni Rais haito saidia. Kikubwa ni nchi yetu sote tusikae kufatilia vitu vidogovidogo visivyo jenga jamii. Tuwe wabunifu tujenge Taifa letu. Hapo ulipo jiulize umefanya nini kwa jamii. Siyo kukashifu kupinga. Hivi hata tukifa Mungu akakuuliza nilikuweka duniani nini ulifanya jibu hakuna. Tukosoe kwa kuwa na mawazo mbadala yatakayo leta ufanisi kwa jamii. Je rais kuongea vile kaathiri imani ya mtu?
Umeeongelea Kuhusu issue za kitaifa pale kaongelea issue za Taifa. Unaposema issue ikihusu ulevi ikaongelewa bar unanishitua kidogo. Mfano baba akiwa na mtoto mlevi atamchukua wakaongelee bar. Kama hatahitaji mkanya mtoto juu ya ulevi. Wazazi wengi hata akikosea mtoto mmoja. Mfano ni mlevi mara nyingi mzazi uweka kikao cha familia ili kuweka funzo kwa watoto wote. Corona ni issue ya Taifa na kimataifa, kilichoongelewa pale ilikuwa kwa manufaa ya Taifa.
Ubarikiwe,
Wasalaam Walykum!
NB: TUENDELEE KUMTEGEMEA MUNGU ATUVUSHE KATIKA HILI PIA TUSISAHAU KOMBEO ZETU WAKATI WA KUPAMBANA NA GOLIATH MAAN TUKIMKABIDHI MUNGU HIZO KOMBEO HUWA HATARI KULIKO PANGA LA GOLIATH. AMEN.
Sent from my SM-J111F using JamiiForums mobile app