Rais Magufuli ahutubia wana Kagera: Aitaifisha shule ya Omumwani inayomilikiwa na CCM

Magazetini

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
588
1,698


Habari wakuu,
Tuwe pamoja kujuzana yanayojiri Bukoba ambapo Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anahutubia wakazi wa Bukoba na watanzania kwa ujumla.

======

UPDATE

Magufuli: Cement imechangwa zaidi ya 30,600 na mabati zaidi 31,000. Wananchi wameshaanza kupewa, wengine wamejengea na wengine wameuza.

Kamati ya maafa Mkae na mfahamu kila senti imeenda wapi, kuna pesa haionekani imetumika wapi.

Magufuli: Hatutajenga nyumba za wananchi, hakuna sehemu yeyote duniani tetemeko likitokea, serikali inajenga nyumba za wananchi. Nyumba zimebomoka zaidi ya 2,000.

Rais Magufuli ametaifisha shule ya Omumwani inayomilikiwa na Jumuiya ya wazazi(CCM) mkoani Kagera.

JAMII LEO


=========

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo Jumatatu Januari mbili, 2017 amemaliza ziara yake ya siku mbili Mkoani Kagera kwa kuwatembelea baadhi ya wananchi walioathiriwa na tetemeko la ardhi pamoja na kukagua baadhi ya miundo mbinu iliyoathiriwa na tetemeko hilo na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa majengo ya shule ya sekondari ya Ihungo Omumwani iliyobomolewa na tetemeko la ardhi la Septemba 10,2016.

Mara baada ya ukaguzi huo Rais Dkt Magufuli akazungumza na wananchi wa Mkoa huo wa Kagera katika viwanja vya Shule ya Sekondari ya Ihungo na kuagiza kuvunjwa kwa kamati ya maafa ya Mkoa huo iliyokuwa ikiratibu utoaji wa misaaada na kufanya tathmini ya athari ya tetemeko hilo.

''Kila kitu huwa kina mwanzo na mwisho wake ukiwa na harusi huwa kuna kamati ya harusi,ukishamaliza kufunga ndoa kamati ya harusi huwa inavunjwa,na ukiwa kwenye msiba huwa kuna kamati ya msiba na msiba mkishazika kamati ya mazishi huvunjwa,kamati ya maafa ya Kagera huu ni mwezi wa tano na inawezekana hata kwenye kamati huwa wanalipana posho,sasa nataka hii kamati nayo iishe,yalishapita yamepita''

Aidha Dkt Magufuli amewataka wote walioahidi kuchangia katika kamati ya tetemeko la ardhi ya mkoa wa Kagera ambao bado hawajatekeleza ahadi zao ambazo ni jumla ya shilingi bilioni nne nukta tano wakamilishe ahadi hizo ili ziweze kumalizia miundombinu ya Serikali iliyoathiriwa na tetemeko hilo.

Ameongeza kuwa wale wote wanaoendelea kuguswa kusaidia wapeleke michango yao moja kwa moja kwa wananchi badala ya kuipeleka serikalini kwa kuwa hakuna mchango mwingine utakaopokelewa katika Ofisi ya Waziri Mkuu.

Pia Rais Dkt Magufuli ameagiza shule ya Sekondari ya Omumwani iliyokuwa inamilikiwa na Jumuia ya Wazazi wa Chama Cha Mapinduzi CCM imilikiwe na Serikali kutaka wanafunzi wote wanaosoma katika shule hiyo kutolipa ada kama zilivyo shule nyingine za serikali.

Dkt Magufuli ameuagiza uongozi wa Mkoa wa Kagera kupunguza utitiri wa kodi katika zao la kahawa ili bei ya zao hilo ipande na kuwanufaisha wakulima

Balozi wa Uingereza hapa Nchini Bi Sarah Cooke ambaye nchi yake imechangia kiasi cha shilingi bilioni sita kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Ihungo, amempongeza Rais Dkt Magufuli na serikali yake kwa jitihada za kupambana na rushwa suala ambalo nchi yake ya Uingereza inalipa kipaumbele sambamba na kutoa elimu bila malipo jambo linalowawezesha watoto wengi wa kitanzania kupata elimu bure

Jaffar Haniu

Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Kagera.

02 Januari, 2017
 
IMG-20170102-WA0052.jpg
 
Magufuli: Nataka niwapongeze wahisani kwa kuchangia maafa ya Kagera. Zile bilioni sita za Uingereza tuliamua zikajenge shule na shule itakuwa kama Ulaya. Anapendekeza shule hiyo iitwe "Tetemeko secondary school"

Magufuli: Tuliamua kuwa kuwa shule zikasaidie miradi itakayotumika na wana Kagera wote. Tuliamua tusigawe kwa wananchi.

Pia ametangaza rasmi kutaifisha shule iliyokuwa ikitumika na CCM kuwa ya serikali. Kama kuna madai watalipwa. Ametoa "Insruction" kwa waziri Ndalichako kuanza mchakato huo mara moja!
 
Naona yanajirudia tu yale yale ya "hatutajenga nyumba za wananchi, watu wasijinufaishe na misaada. Sijui nimekaa kwenye konstiraksheni indasitiry kwa zaidi ya miaka 20. Sijui hakuna nchi yoyote duniani serikali ikaanza kujenga nyumba za wananchi kwenye majanga.. Naona amerudi kwenye majizi na mafisadi

Namuacha aendelee kuongea mimi naambaa ambaa kama mwewe!
 
Back
Top Bottom