figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,481
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa John Pombe Magufuli amefuta hati ya mashamba ya Mkonge, yenye hekta zaidi ya 5000 yaliyokuwa yametelekezwa na kuwa mapori ambayo hayaendelezwi kufuatia malalamiko ya wakazi wa zaidi ya 2000 wa kijiji cha Kibaranga kuhangaikia maeneo ya kilimo na kusababisha migogoro ya mara kwa mara baina yao.
Akizunguza na wananchi wa kijiji cha Kibaranga katika mkutano wa hadhara,waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi Mheshimiwa William Lukuvi amesema hili ni shamba la tano kufuntwa na Mheshimiwa rais katika mkoa wa Tanga kufuatia wawekezaji waliopewa hati ya kuyaendeleza kushindwa kutekeleza makubalino.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Tanga Martin Shigella amesema serikali mkoa wa Tanga imepewa jukumu la kugawa ardhi hiyo watahakikisha kuwa wanaweka utaratibu utakaowezesha kuwa kila mwananchi apate shamba na hati ili yaweze kuwaendeleza wananchi.
Kufuatia hatua hiyo mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoshughulikia ulinzi na usalama Mheshimiwa Adad Raja amesema watahakikisha wawekezaji matapeli hawaruhusiwi kujimegea ardhi kwa manufaa yao na badala yake mashamba hayo yaendelezwe na wananchi waliokabidhiwa ili yaweze kuwapa manufaa.