Rais Magufuli afungua Msikiti Sumbawanga, awashukuru waislamu kwa upendo wao wa kumualika

alexelias

JF-Expert Member
Sep 1, 2017
2,032
3,198
Rais Magufuli amefungua msikiti wa Sumbawanga na kuwataka waislamu kuendelea kuwa wamoja na kudumisha upendo miongoni mwao na kwa wale wasio waislamu.

Kadhalika Rais Magufuli amewashukuru waislamu kwa kumpa heshima ya kufungua msikiti huo na kusema huo ni upendo wa dhati ikizingatiwa kuwa yeye ni mkristo.

Katika ufunguzi wa msikiti mpya wa bomani huko Rukwa,Sumbawanga mjini Rais Magufuli amemtaka mlinzi wake aombe kwa ajili ya kusanyiko lile.
 
Rais ni mnyenyekevu na anawapenda wasaidizi wake
 
Nimeona nije kwa kutaka kujua kama dini yetu ya haki inaruhusu mtu asiye muislamu kuzindua msikiti

Nimeona muda mfupi uliopita hata mkoani Rukwa mh rais wetu akipewa dhamana kubwa ya kutuzindulia msikiti wa istqwaama hapa bomani

". Maendeleo hayana vyama"
 
Ukiona ameruhusiwa na hao viongozi wako kuuzindua huo msikiti, basi utambue hiyo dini yenu inaruhusu utaratibu wa aina hiyo. Una swali lingine?
 
Shabiki wa mtu, leo umepatikana?

Hakuna shida maana anaishia nje tu, hasalishi wala kufanya chochote ndani zaidi ya kukata utepe
 
Back
Top Bottom