Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 2,807
- 11,969
Salaam wakuu,
Rais Magufuli afanya ziara ya Kikazi Mkoani Kagera huko mpakani mwa Tanzania. Itamchukua Siku tatu kuuzunguka Mkoa huo
Pamoja na mambo mengine Keshokutwa kusainiwa mkataba mkubwa unaohusu mgodi wa madini ya Nickel yaliyopo Kabanga Rulenge Wilaya ya Ngara.
Rais Magufuli kasema Mkataba huu ni wa Mabiloni ya hela, amesema anasaini mkata huo ili Watu wa Kagera Wapate ajira.
Akiwa Muleba raia Magufuli amehimiza Kilimo sababu nchi imeingia Uchumi wa Kati. Ataka watu walime ili wawauzie wale wanaojifungia ndani sababu ya Corona