Rais Magufuli afanya ziara Benki Kuu, aongea na uongozi

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Bot1.jpeg

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli akiongeza na uongozi wa juu wa Benki Kuu pamoja na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt Philip Mpango na Katibu Mkuu wake Dkt. Servacius Likwelile alikofanya ziara ya kushtukiza makao makuu ya BOT jijini Dar es salaam leo Machi 10, 2016

bot4.jpeg

bot5.jpeg


=================


VIDEO: Rais Magufuli akionesha majina ya wafanyakazi hewa BoT

Rais Magufuli akiwaonyesha wakuu wa BOT majina ya wafanyakazi hewa ambao uongozi umekiri kufanya makosa na kuahidi watarekebisha mara moja kwa kuyaondoa kwenye vitabu vya BoT.

Rais amewaamuru wayaondoe mara moja ili pesa zitumike kulipa wafanyakazi wanaostahili kulipwa kama wafanyakazi wa BoT ili wanufaike na matunda ya kazi zao.

Rais amesitikishwa na uzembe na pia wizi unaofanyika BoT kwa njia za udanganyifu.

Rais hakuishia hapo tu bali ameiagiza pia Benki hiyo kusitisha mara moja ulipaji wa malimbikizo ya malipo ya shilingi Bilioni 925.6 ambayo tayari yalishaidhinishwa na badala yake yarejeshwe Wizara ya fedha na Mipango kwa ajili ya kufanyiwa uhakiki.

Alichokifanya Rais Magufuli ni kile Waingereza wanasema, He caught BoT top brass with their pants down!



Angalizo:
Hili suala linaweza kuonekana kwa wengine ni dogo lakini implication yake ni kubwa sana kwa taifa. Hii inatueleza hazina ya taifa haiko salama, kitu ambacho ni hatari sana kwa usalama wa Taifa.

Kama wanaweza kuwa na majina ya wafanyakazi hewa, siyo ajabu wakawa na pia wafanyakazi wasiokuwa na ujuzi wa kazi wanazozifanya, kitu ambacho ni hatari kiuchumi kwa ustawi wa taifa.

Kama na Bank of Tanzania(BoT) inaweza kufanya madudu kama haya ambayo mara nyingi yanafanywa na wahasibu wa halmashauri, sina budi kukubaliana na maneno ya Rais Magufuli wakati akiongea na wananchi wa Arusha aliposema,
 
Yeah, ni asubuhi na alikutana na management yote ya Benki Kuu.
 
Tunataka ziara ya kushtukiza wizara ya Muungano na mazingiraAtaongea nini na Makamba?
 
naona kale kajipu ka riba za mabenki kanataka kutumbuka, yule mama si aliambiwa atoe majibu ndani ya siku tatu naona alipuuzia.
 
tusubri kipele kikikunwa maana hakuna jipu kwa nyuso hizo hapo juu.
 
Mwenye taarifa ya walichoongea wakuu.......tujue angalau wamemuambiaje khs kuimarika kwa shilingi yetu?
 
Back
Top Bottom