The Sheriff
JF-Expert Member
- Oct 10, 2019
- 613
- 1,776
Rais Magufuli amefanya uteuzi wa wenyeviti 3 watakaoongoza bodi za taasisi mbili za serikali na moja ya ubia wa serikali na sekta binafsi, ambapo kwa mujibu wa taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi Mh. Balozi John Kijazi, uteuzi huo umeanza jana tarehe 30 Januari,2020
Rais amemteua Bwana Gabriel Pascal Malata ambaye ni Naibu Wakili Mkuu wa Serikali kuwa Mwenyekiti Mjumbe wa kuiwakilisha serikali katika Bodi ya Kampuni ya Airtel Tanzania Ltd.
Aidha, Amemteua Prof. Martha Qorro, ambaye ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi wa Chuo cha Mipango na Maendeleo Vijijini (Institute of Rural Development Plan – IRDP)
Uteuzi wa tatu ni wa Prof Joseph Rwegasira Buchweshaija kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST)