Rais Magufuli afanya uteuzi wa Makamishina wa Jeshi la Polisi

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,272
47,268
Mkuu wa Majeshi ya Polisi, IGP akutana na wanahabari muda huu, fuatilia kinachojiri.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP) Simon Sirro amefanya mabadiliko ya kiuongozi kwa maofisa wa jeshi hilo baada ya Rais John Magufuli kufanya uteuzi wa makamishna wapya.

Akizungumza na vyombo vya habari leo Machi Mosi, IGP Sirro amewataja makamishna walioteuliwa na Rais Magufuli kuwa ni Charles Mkumbo ambaye anakwenda kuongoza kamisheni ya intelijensia na Liberatus Sabas ambaye anakuwa mkuu wa operesheni na mafunzo.

Wengine ni Leonard Lwabuzala ambaye ataongoza kamisheni ya fedha na logistics na Benedicto Wakulyamba ambaye anakuwa mkuu wa kamisheni ya utawala na menejimenti ya utumishi na Shaaban Mlai ambaye ataongoza kamisheni ya maabara ya uchunguzi wa kisayansi.

Mbali na makamishna hao, Sirro amefanya mabadiliko ya kiutawala kwa maofisa wa jeshi hilo; James Mushi ambaye alikuwa kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma anakuwa Mkuu wa Chuo cha Polisi (CCP) Moshi wakati RPC wa Njombe, Renata Mzinga akirudishwa Makao Makuu.

Sirro amewataja makamanda wapya wa mikoa kuwa ni Amon Kakwale (RPC wa Temeke), Jonathan Shana (RPC Arusha), Marwa Mahiga (RPC Ruvuma), Salum Hamduni (RPC Njombe) na Zuberi Chembela (RPC Ilala).

Viongozi wengine waliohamishwa vituo vya kazi ni Mihayo Nsekela (ofisi ya operesheni na mafunzo), Simon Haule ambaye alikuwa RPC wa Shinyanga anarudishwa Makao Makuu na Yusuph Sarungi ambaye alikuwa RPC Songwe anakuwa mkuu wa kitengo cha kushughulikia wizi wa mifugo (SPU).

Benedict Mapugila ameteuliwa kuongoza kikosi cha bandari wakati Michael Marwa anapelekwa makao makuu Zanzibar. Sirro amesema Albert Nyamhanga na Nsato Marijani wanakwenda Idara ya Wakimbizi ambayo iko chini ya Idara ya Uhamiaji.
 
Yule wa nyakua nyakua muda wake ulikuwa sasa vinginevyo ataendelea kujitathmini milele.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom