Rais Magufuli afanya uteuzi wa Mabalozi, Wakuu wa Mikoa, Makatibu & Manaibu Katibu: Wamo Mnyeti, Mangu, Kashilila..

Kabla ya uchaguzi mkuu mwaka 2015 kwenye gazeti la Mawio, kuna mtaalamu mmoja alichambua "afya ya akili" ya mgombea mmoja akahitimisha kwamba, mgombea huyo kama ikishinda, kuna siku atafanya uamuzi ambao utaligharimu mno taifa hili. Kuna watu wanasema kwenye korido mbalimbali kwamba hiyo ndio sababu hasa ya gazeti hilo kufungiwa!
Mlikuwa nae ndani ya ccm, pamoja na polisiccm lakni mkamwacha.
 
Tuna wapinzani wa ajabu zaidi kwa kukubali kumteua fisadi kugombea urais ambapo kwa miaka mingi wakituaminisha ni fisadi asiyesafishika.
Yaani mlilobakisha ninyi lowminded people ni kumtaja Lowasa ilikuficha upu.mbavu wenu. Kama lowasa ni fisadi mpelekeni mahakamani, sasa kuna mahakama ya mafisadi mnasubiri nini?
 
Kama CCM wameshindwa kupanga mitaro, wataweza nini?,Mungu awalinde wanaopatwa na adha ya mafuriko.

Nakumbuka jinsi Dar es salaam na majiji mengine yalivyokuwa kimya! huku sauti ya Lubuva ikitawala anga la pwani ya mashariki ya Africa, siku ile hata ndege hawakuruka kwa simanzi.

Hakuna haja ya kumshangaa Magufuli kwa kuwaongezea vyeo akina Mnyeti. Huwezi kutegemea jambo tofauti kutoka kwa Magufuli. Ni mtu anayefanya 'sentimental judgement' kwa lengo la kukidhi hisia zake dhidi ya watu anaowachukia na kwa kuwafurahisha wanaomfurahisha katika ulimwengu wa chuki zake, bila kujali maamuzi hayo yana 'impact gani kwa ujumla wa kitaifa'. A lowly mind in the high office.

'Kiongozi dhaifu kabisa ni yule anayeshindwa na nguvu za hisia zake'

Niliposikia Mtuhumiwa Wa Rushwa Kateuliwa Kuwa Mkuu Wa Mkoa Nikakumbuka Kauli Ya Tundu Lissu Kuwa TUNA RAIS WA AJABU HAIJAWAI KUTOKEA !!

mr mkiki.
Watanzania tulimkataa mtuhumiwa wa ufisadi aliyepewa nafasi Na chadema kugombea urais 2015
 
Na yule aliyevamia shamba la mtu na kung'oa mazao nadhani kaukwaa uRC pia. JPM banaa
 
Tuna wapinzani wa ajabu zaidi kwa kukubali kumteua fisadi kugombea urais ambapo kwa miaka mingi wakituaminisha ni fisadi asiyesafishika.
Nyie Lowassa atawapindisha kibyongo. Unaposema kugombea ni tofauti na kiongozi wa nchi. Suala la Lowassa linawahusu watu wa CHADEMA peke yao wakati suala la uteuzi wa Mnyeti linaleta utata kuhusu nini hasa maana ya maadili kwenye nchi yetu.

Wewe ni mara ngapi umesikia watu wakisimamishwa kazi kwa tuhuma za ufisadi? Halafu Kikwete akiwa Rais alishasema Lowassa siyo fisadi!
 
Rais Magufuli amemteua aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Arumeru, Alexander Pastori Mnyeti kuwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara.

Hapo awali Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari na yule wa Arusha Godbless Lema, walimtuhumu Mnyeti kutoa rushwa katika Vitendo vya kununua madiwani wa CHADEMA
Kapongezwa na mkuu inaonekana alitumwa kazi hiyo
 
Nicolaus .b.w.mkapa ......naona wamechaguana kweli nchi hii keki inaliwa na wenyewe

Ova
 
Mambo mengine jamani tuweke tu itikadi pembeni, hivi kweli kiongozi aina ya Alexander Nyeti ni vipi atamsaidia Rais wetu pendwa kufikia malengo?
Kiongozi ambaye ameonekana wazi kufanya ujanja ujanja kutafuta waungaji mkono kwa kutumia pesa za umma bado tumwamini tu kuendelea kuwepo madarakani?

Kwa hapa Mh Rais ameniangusha sana hasa pale ambapo aliapa kula sahani moja na watoa au wapokea lushwa, Sidhani kama tuna nia njema kupambana susala hili kabisa kwa kumuogopa Mungu.

Kimaadili Mnyeti alifanya kosa kubwa sana, hatakiwa kuaminiwa kua viongozi wa umma. Tume ya maadili ya uongozi wa umma sijui ni kwanini ilikua na kigugumizi juu ya hili?

Wanaccm mnaweza kulichukulia kama jambo jema sana kipropaganda lakini ni hatari sana kiutendaji na kufikia malengo. Muda ni mwalimu mzuri sana.Kiongozi wa aina hii kuendelea kumpa mamlaka zaidi kwenye ofisi za umma ni kuzidi kumpa nafasi ya kuharibu zaidi.
Hata mZinzi akitubu anaiona mbingu sembuse huyu yuko duniani

[HASHTAG]#pambananahaliyako[/HASHTAG]
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom