mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,076
- 4,113
Rais Magufuli amemteua Dkt. Jumanne Fhika kuwa RC wa Njombe akichukua nafasi ya Christopher ole Sendeka. Kabla ya kuteuliwa Dkt. Fhika alikuwa Ofisi ya Rais.
Dkt. Aloyce Nzuki ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, anachukua nafasi ya Prof. Adolf Mkenda.
Rais Magufuli amemteua Dkt. Allan Kijazi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili. Dk. Kijazi pia ataendelea kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Mhandisi Anthony Sanga ameteuliwa na Rais kama Katibu Mkuu Wizara ya Maji, nafasi ambayo ilikuwa inashikiliwa na Prof. Kitila Mkumbo. Rais Magufuli amemteua Mhandisi Nadhifa Kemikimba kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo.
Aidha, Fadhili Mohamed Juma ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Geita akichukua nafasi ya josephat Paulo Maganga ambaye amehamishwa kituo. Kabla ya uteuzi huo, alikuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoani Lindi.
Josephat Paulo amekuwa Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, nafasi ambayo hapo awali ilikuwa chini ya Patrobas Katambi