Rais Magufuli afanya mazungumzo na Wataalamu wa ujenzi wa Uwanja wa michezo Dodoma

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,454
3,418
Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu wa Tanzania na Misri wanaoshughulikia ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI.

Balozi wa Morocco nchini aliyeongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco, Abdelilah Benryane amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocco wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco hapa nchini mwaka 2016.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Msikiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) unaojengwa Jijini Dar es Salaam na kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Patrick Mfugale amesema uwanja huo utajengwa eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma–Morogoro kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 85,000 na 100,005
IMG_20190313_182732.jpeg
IMG_20190313_182727.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na timu ya wataalamu wa Tanzania na Misri wanaoshughulikia ujenzi wa uwanja wa michezo katika Jiji la Dodoma, unaotarajiwa kujengwa kwa msaada wa Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI.

Balozi wa Morocco nchini aliyeongoza ujumbe wa wataalamu kutoka Morocco, Abdelilah Benryane amesema pamoja na kuzungumzia uhusiano mzuri wa Tanzania na Morocco wamejadiliana kuhusu utekelezaji wa miradi iliyokubaliwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco hapa nchini mwaka 2016.

Miradi hiyo ni pamoja na ujenzi wa Msikiti wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata) unaojengwa Jijini Dar es Salaam na kuanza kwa ujenzi wa uwanja wa mpira wa miguu Jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) Patrick Mfugale amesema uwanja huo utajengwa eneo la Nanenane kando ya barabara ya Dodoma–Morogoro kwa mfano wa mlima Kilimanjaro na utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 85,000 na 100,005View attachment 1044867View attachment 1044869

Sent using Jamii Forums mobile app
Chadema vipi mtajadiliana na wataalamu lini kuhusu ujenzi wa makao makuu ya chadema?
 
Back
Top Bottom