1974hrs
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 741
- 536
Kwa mujibu wa historia, Zaidi ya miaka 1937 imepita kutoka kuzaliwa mmoja wa Wanafunzi wa Kiongozi wa Umma wa Kiislamu Mtume Muhamad (S.A), Imamu Ally ambaye katika kipindi cha uongozi wake alisifika zaidi kwa mambo makuu manne.
Moja ya jambo kubwa alilosifiwa katika utawala wake ilikuwa ni utawala uliojaa na imani ya kumuamini Mungu na kumtegemea kwa kila kitu, kwa mujibu wa mapokeo ya Dini ya Kiislamu imeandikwa kuwa mtu mwenye hofu ya Mungu huwa makini sana na jambo lake; kuhusu jambo la Ufisadi Mwanafunzi huyo wa Mtume alilipiga vita wakati wa utawala wake.
Mambo hayo mawili yanamfanya Kiongozi Mkuu wa Waislamu wa Dhehebu la Shia la Ithnasheri ya Tanzania Sheikh Hemed Jalala kumfananisha kwa kiasi kikubwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli katika kila jambo kwenye utawala wake.
Wakati leo ikiwa ndio kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu huyo Sheikh Jalala ameeleza jambo lingine ambalo lilikuwa katika Serikali yake ilikuwa ni uwajibikaji ambao kwa sasa ubeti mkubwa wa Rais Magufuli ni #HAPA KAZI TU katika dhana ya Uwajibikaji.
Unaweza kusikiliza hapo chini sauti ya Sheikh Jalala akiufananisha utawala wa Imamu Ally na wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli.