Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,137
Ziara ya mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, inaendelea katika Mkoa wa Pwani ambapo ametoa tamko zito kwa wakazi wa Kibiti na Rufiji na kueleza kwamba watachelewa kupata maendeleo, ikiwemo kujengwa kwa viwanda, kwa sababu ya vitendo vya uhalifu na mauaji.
Rais Magufuli amesema wananchi wa Rufiji na Kibiti wanawajua wahalifu lakini wanawaficha na kukataa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo.
Akawatahadharisha wote wanaoendeleza vitendo vya mauaji ya viongozi wa serikali, chama na askari Kibiti, Mkuranga na Rufiji kwamba serikali yake siyo ya kuchezewa, atahakikisha wananyooka. Akawataka kama wanamsikia, wapeleke salamu kwa wenzao kwamba serikali yake siyo ya mchezo.