Rais Magufuli Achimba Mkwara Mauaji Kibiti na Rufiji, Asema Watanyooka

Hashpower7113

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
1,260
2,000
Ziara ya mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, inaendelea katika Mkoa wa Pwani ambapo ametoa tamko zito kwa wakazi wa Kibiti na Rufiji na kueleza kwamba watachelewa kupata maendeleo, ikiwemo kujengwa kwa viwanda, kwa sababu ya vitendo vya uhalifu na mauaji.

Rais Magufuli amesema wananchi wa Rufiji na Kibiti wanawajua wahalifu lakini wanawaficha na kukataa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo.

Akawatahadharisha wote wanaoendeleza vitendo vya mauaji ya viongozi wa serikali, chama na askari Kibiti, Mkuranga na Rufiji kwamba serikali yake siyo ya kuchezewa, atahakikisha wananyooka. Akawataka kama wanamsikia, wapeleke salamu kwa wenzao kwamba serikali yake siyo ya mchezo.

Cannibal OX

JF-Expert Member
Aug 27, 2014
2,720
2,000
Nafikiria tu haya mauaji ya Pwani kama vile Kibiti et al.... sijui ni hujuma zinafanywa na Watu wanaompinga Rais JPM hasa katika Sera ya Viwanda plus Ufisadi in general?

Wanaharibu amani katika Eneo hilo ili Wawekezaji wasiende? Pwani inaweza kuwa Case Study ya Sera ya Viwanda awamu ya Tano kama hizi jitihada zikizaa matunda. Only time will tell.
 
ng'adi lawi

JF-Expert Member
Sep 27, 2014
2,955
2,000
Ziara ya mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli, inaendelea katika Mkoa wa Pwani ambapo ametoa tamko zito kwa wakazi wa Kibiti na Rufiji na kueleza kwamba watachelewa kupata maendeleo, ikiwemo kujengwa kwa viwanda, kwa sababu ya vitendo vya uhalifu na mauaji.
Rais Magufuli amesema wananchi wa Rufiji na Kibiti wanawajua wahalifu lakini wanawaficha na kukataa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama, jambo ambalo linarudisha nyuma maendeleo.
Akawatahadharisha wote wanaoendeleza vitendo vya mauaji ya viongozi wa serikali, chama na aksri Kibiti, Mkuranga na Rufiji kwamba serikali yake siyo ya kuchezewa, atahakikisha wananyooka. Akawataka kama wanamsikia, wapeleke salamu kwa wenzao kwamba serikali yake siyo ya mchezo.
Ardhi yote ya Tanzania ni Mali ya umma chini ya rais. Kama hawataki kushirikiana na serikali hao wakorofi walipwe fidia na kuhamishwa vijengwe viwanda.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
186,769
2,000
Nafikiria tu haya mauaji ya Pwani kama vile Kibiti et al.... sijui ni hujuma zinafanywa na Watu wanaompinga Rais JPM hasa katika Sera ya Viwanda plus Ufisadi in general?

Wanaharibu amani katika Eneo hilo ili Wawekezaji wasiende? Pwani inaweza kuwa Case Study ya Sera ya Viwanda awamu ya Tano kama hizi jitihada zikizaa matunda. Only time will tell.
Hizi hisia ndiyo saratani yetu
 
Mr. Bigman

JF-Expert Member
May 7, 2011
2,557
2,000
Unawezaje kumtumia salamu adui ambaye humfahamu? Hivi Rais anaongea na akina nani hasa walioko kibiti?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom