Rais Magufuli acha kutembelea nchi masikini hazitakusaidia chochote

Tajiri Tanzanite

JF-Expert Member
Oct 23, 2016
2,069
3,705
Hapo vip!!
Binafsi Ziara za Rais wetu muheshiwa Dr. John Pombe Magufuli, naona kama ziara ambazo hazina maslahi kwa Taifa letu.

Nchi anazotembea ni maskini yenye matatizo kama ya nchi yetu au hata zaidi ya nchi yetu.
Tafsiri yake anatumia Pesa za wananchi bure kwenda kuzura na kuwatembelea maskini wenzake wasioweza kumsaidia wala yeye kuwasaidia, kwa ujumla ni ziara za kimaskini,ambazo hazina maslahi kwa nchi yetu.

Ni wazi uchumi wa nchi yetu ipo ICU, tunaitaji ziara zinazoweza kuleta uvumbuzi dhidi ya matatizo ya uchumi yanayoikabili nchi yetu.

Najaribu kujiuliza katika hizo nchi anazotembelea, tunaweza kuwapata wawekezaji, wakuja kuekeza katika nchi yetu..?

Ziara katika nchi tajiri Kama za America na Ulaya ni muhimu na hazikwepeki kufanywa na Rais nchi yetu, sasa yeye anatembelea Mataifa maskini,sio kosa kutembelea nchi za kiafrika ila atambue hizo ziara hazina maslahi Sana kwa Taifa letu kwa sasa.

Ni wazi nchi yetu bado inahitaji misaada, sio Swala la kumumunya maneno hapa, sasa katika hizo nchi anaweza akapata vip misaada, habari ya kujidai maskini jeuri huku huna mbinu mbadala za kutatua tatizo ni kujitesa mwenyewe.

Akafanye ziara Duniani huko, ziara za kuwatembelea wakina Museveni, Kagame na wengine wanaofanana nao, hazina tiga kwa maslahi Sana kwa nchi yetu.

Robert Mugabe alijidai maskini jeuri, Lakini wote nyie ni mashahidi kwa kilichoikumba uchumi wa Zimbabwe..

Kwa maoni yangu kuliko angefanya hizo ziara bora angebaki tu Ikulu.
 
Partly ninakubaliana na wewe na partly sikubaliani pia. Kuna nchi zingine ni masikini wenzetu lakini ni strategic sana kwetu.

Mfano unaendaje Namibia kufungua kibarabara then kwa wachovu wengine kama Zimbabwe halafu unaacha kwenda DRC ambako 70% ya transit goods za bandari ya Dar ni za kwao?

Tuliboronga kwenye kuapishwa kwa Felix nikajua tungeitumia hii nafasi ya South Africa ambako Felix alikuwepo plus kavisit fulani hivi ili kurekebisha kidogo alipoharibu Uhuru.

Kwa zile picha nilizoziona I doubt hata kama presidia wetu alisalimiana vzr na Felix Tshisekedi ambaye ni mdau mkubwa kiuchumi kwetu kama nchi kuliko hizo nchi nyingine zote.

Zambia pia ni strategic kwa sababu ya matumizi ya bandari yetu plus mambo mengine mengi. Namibia na Zimbabwe ni wadau wa kihistoria zaidi so siyo beneficial kivile kiuchumi.

Kwenda Namibia na Zimbabwe halafu ukaacha Zambia na DRC ni bonge la mistake.

Kwa mara nyingine Profesa wetu Kabudi anaendelea kuthibitisha kwamba huenda yeye ni mwalimu mzuri lakini si kiongozi mzuri kama alivyodhirisha wazi kwenye issue ya Indo Power.
 
Back
Top Bottom