tajirijasiri
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 2,863
- 3,851
Mh, Magufuli, achana na utumiaji wa nguvu nyingi kulazimisha matukio yatokee badala yake, jikite kwenye kulazimisha mfumo mpya ndani ya Serikali.
Mfano. Badala ya kulazimisha Polisi wazuie Shughuli za Vyama vya Siasa ambazo ni halali kwa mujibu wa Katiba, jikite kujenga Mfumo wa Demokrasia, utakaowawezesha wananchi na wanasiasa kushindana kwa nguvu ya hoja.
Badala ya kulazimisha watu kulipa kodi, jikite katika kujenga mfumo utakaowawezesha walipakodi kulipa kodi kwa hiari bila shuruti.
Badala ya kulazimisha watu kuchangia madawati, tengeneza Mfumo utakaowezesha upatikanaji wa madawati kwa kodi wanazolipa wananchi.
Badala ya kulazimisha wafanyabiashara waache kuagiza sukari, weka mfumo utakaowaruhusu wafanya biashara kuingiza sukari yenye ubora.
Badala ya kulazimisha kuzuia matangazo ya Bunge live ambayo ni kinyume na Haki ya kikatiba ya kupata habari na kinyume na sera ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) jikite kujenga mfumo utakaowawezesha wananchi kupata Habari nyingi zaidi juu ya utendaji wa serikali yao, ikibidi hata kwa simu za viganjani live.
Siku zote Ulazimishaji wa Matukio ni wa Msimu, lakini Ulazimishaji wa Kujenga Mfumo mpya ni endelevu.
Nawasilisha.