Rais Magufuli acha dhihaka

My Son drink water

JF-Expert Member
Nov 30, 2016
4,932
13,283
Dunia nzima inajua kuwa Tanzania mikononi mwako haina Demokrasia ,umefanya kila unaloweza kuua Demokrasia na Uhuru wa Habari.

Mimi hapa nakuandikia nikiwa natumia ID fake ili kulinda usalama wangu.

Lakini jukwaa hili la Jamiiforums nalotumia linaandamwa na serikali ili litoe siri au majina halisi ya wakosoaji wa serikali humu, na hadi sasa Kesi ipo mahakamani.

Wewe ni mkuu wa nchi, mfalme wa taifa la Tanzania, kutamka kwako hadharani kwamba eti Tanzania ina Demokrasia kubwa, ni kuwadhihaki watu wako uliowanyima haki yao ya kikatiba ya kuchagua viongozi wanaowataka.

Nikueleze wazi kwamba tangu umeingia madarakani umesahau kabisa kuwa maisha yana kesho, leo hii wewe ni Rais ila siku zijazo hutakuwa Rais tena, na hawa wanaokupa sifa kila siku hata ambako hustahili watakugeuka wote na kuanza kumsifia Rais atakayekuwa madarakani.

Mh Rais, hofu yako iko wapi hasa? mbona kuna sehemu unafanya vizuri kiasi cha kukubalika na watu automatically? Kwanini umekubali kuchoreshwa kiasi hicho?

Yaani wewe ni Binadamu, una mapungufu mengi tu sasa iweje ukubali kusifiwa kiasi hicho na wanaokukosoa waonekane wabaya?

Mwl Nyerere aliulizwa swali na mwandishi wa BBC enzi za uhai wake akiwa Rais mwaka 1983.
"Why are you getting ready to retire? "
Mwl Nyerere alijibu.

"Because I need to create a fresh legacy of mine and my country as well ".

Leo hii watanzania tunajivunia Mwl Nyerere, hata mabeberu walimpenda na kumwogopa Mwl.
Nyerere aliwahi kumshauri Kaunda na kumwambia.

"Mzee mwenzangu, achia madaraka kabla watu hawajakuchoka ".

Kaunda alikuwa Kiburi, hakuwa na hekima, hakusikiliza ushauri wa Mwl, matokeo yake alikuja kuondoka madarakani kwa aibu kubwa mno.

Wazambia hawana Rais wa kujivunia Kama sisi watanzania tunavyojivunia kwa Nyerere.

Ni kwa sababu Kaunda hakuacha Legacy nzuri.
Kikwete ameondoka madarakani na kuacha Legacy ya kuheshimu mfumo wa vyama vingi na Demokrasia.

Miaka ya nyuma Kati ya 1980 au 1984 Tanzania ilikumbwa na balaa la njaa, Nyerere hakuwaambia watanza nia kwamba ni wavivu na hawalimi watakufa njaa...

Alikimbilia Marekani kuomba msaada wa Chakula kwa ajili ya watu wake, msaada ulikuja haraka na malori yakaanza kusambaza Chakula nchi nzima, kila kaya iligawiwa Chakula cha kutosha, Mahindi ya njano, Burga (American meal) Maziwa ya unga pamoja na mafuta ya kupikia.

Wananchi walikula na kusaza hadi balaa la njaa lilipoisha .

Je wewe utaacha Legacy gani kwa taifa lako?
Rejea ya Tetemeko la Bukoba, MV Nyerere, Wafanyakazi, Demokrasia na Uhuru wa Habari, Uchumi wa nchi na anguko kuu la Mihimili ya Serikali.

=====
Maoni ya Wadau
My son Drink Water naweza kukubaliana nawe kwenye kiini na dhamira ya uzi wako lakini napenda nitofautiane nawe kwenye baadhi ya facts ulizozileta ku support argument yako hasa kumhusu marehemu Mwalimu Nyerere

Tofauti na ulivosema kwamba Nyerere alimshauri Kaunda aachie ngazi ukweli ni kwamba Mwalimu alimshauri Kaunda asifanye uchaguzi kwa sababu taarifa za ki intelijensia alizokua nazo(na Mwalimu was good at that) zilionyesha Kaunda asingeshinda uchaguzi huo. Hayo ni maneno yake mwenyewe Nyerere na aliyatoa hadharani na kumbukumbu zipo

Kwa maneno mengine(hii ni tafsiri yangu) ni kama alikua anamwambia Kaunda awafanyie ubabe raia wake asifanye uchaguzi!!! Kama ikiwezekana aibe uchaguzi abakie kua Rais wa Zambia ushauri ambao Mzee Kaunda aliukataa, akaingia kwenye uchaguzi akiwa na tume huru kabisa kabisa kabisaaaa ya uchaguzi na matokeo yalipotangazwa aliyakubali bila kinyongo wala hila!

Hii ni legacy aliyoicha Mzee Kaunda ya ku set precedence ya kuheshimu demokrasia na kukubali matakwa ya raia na sauti yao kupitia sanduku la kura na kwa hilo Zambia wametushinda sana.

Kwa taarifa yako tu marehemu Mwalimu Nyerere ndiye alikua championi wa siasa za hila na ubabe wa kichama na ndio muasisi wa katiba tunayoilalamikia sasa na hata yeye mwenyewe baada ya kuachia ngazi kama rais lakini pia ndie fundi mkuu na injinia wa supremacy ya kibabe na ujanja ya Chama Cha Mapinduzi akidaiwa ndie aliyesimamia na ku set precedence ya kupindua matokeo ya chaguzi za Zanzibar (mbinu inayoigwa na Tanzania Bara pia) kwani hakutaka wala hakuamini chama au mtu asiyekua CCM aongoze Tanzania

Aliwahi tu wakati mmoja kumsifia Mandela kwamba ni bora kaondoka mapema madarakani kwani akisubiri azeeke akili inaweza kukataa kuondoka madaralani. Hapa kweli alikua anampiga vijembe Mugabe aliyekua amegoma kuachia wengine wagombee urais wa Zimbabwe

Tofauti yake na waliokuja kumrithi ni uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja, akili angavu ya kuona mbali na hata uadilifu(hakuiibia nchi wala kua na double standards kwa wasaidizi wake). Kiasi kwamba mkono wake wa chuma haukuonekana wala hila zake hazikung'amuliwa mapema!

Pili ni suala la hali ngumu ya kiuchumi iliyoikumba nchi miaka ya mwanzoni ya 1980s hasa baada vita ya Kagera. Ni kweli yaliagizwa mahindi ya Yanga kutoka Marekani lakini si kweli kwamba yalitosheza na kwamba eti watu walikula na kusaza!!!

Kulikua na uhaba wa kila kitu ikiwemo bidhaa zote muhimu kama sukari, sabuni, mafuta ya kula na ya nishati n.k, ambapo zilipatikana kwa foleni na wakati mwingine kwa rushwa na hii ni kutokana na rigidity ya Mwalimu Nyerere kukataa kukubaliana na sera za mashrika ya fedha ya kimataifa na nchi wafadhili/wahisani
 
Unaongelea Mwl Nyerere yupi? Mbona mlimwita haambiliki leo hii nyie tena ndio mmekuwa mstari wa mbele kujitamba kwamba mlikuwa mnamkubali. Bado hatujasahau jinsi mlivyokuwa mnamkebehi leo hii baada ya kufa ndio mnamwona alikuwa mzuri? Hata Magufuli akiondoka baada ya muda wake mtakuja na kusema bora Magufuli angekuwepo, ni binadamu ambao hamna shukrani mmejaa usaliti mioyoni mwenu. Hata muda haujapita kila uchwao mlimsimanga JK ohhh anatembea kama Vasco da Gama etc leo mnamlilia kwa sababu alikuwa hana uwezo wa kuongoza na mlifanya Tanzania dangulo la wauza unga na wezi wa meno ya Tembo nk.

Watanzania wengi hawana shukrani tu pamoja na wewe. Kwanza hufahamu maana ya Demokrasi kwa sababu 1. Demokrasi sio kwa sababu wewe binafsi na kikundi chako cha vikaragosi mna chuki binafsi then mnakuja na ngonjera kusema kwamba hakuna demokrasi. Kwa faida yako na makasuku wenzako tafsri ya Demokrasi hapa chini:

''Democracy is a form of government in which the people have the authority to choose their governing legislation. Who people are and how authority is shared among them are core issues for democratic development and constitution. Some cornerstones of these issues are freedom of assembly and speech, inclusiveness and equality, membership, consent, voting, right to life and minority rights.''

Kama lugha imekupiga chenga shauri yako. Sasa kama wewe umekwazika sema ni lipi hapo ambalo unasema limekukwaza kwa ushahidi sio kuleta viroja kwenye hoja muhimu. Majungu peleka kwa makasuku wenzako.
 
Long Time watumiaji wengi wa Hii forum watumiaji wake wana ID fake tangu tawala za nyuma kwahiyo uongo
 
Nyinyi mashabiki wake Rais, munamupenda sana sana na pia kumuongelea na kumuandika.. mbona hamuja ongelea kiongozi wetu wa nchini.. kiongozi wa upinzani Bungeni!! Hivi yupo pouwa?
 
My son Drink Water naweza kukubaliana nawe kwenye kiini na dhamira ya uzi wako lakini napenda nitofautiane nawe kwenye baadhi ya facts ulizozileta ku support argument yako hasa kumhusu marehemu Mwalimu Nyerere

Tofauti na ulivosema kwamba Nyerere alimshauri Kaunda aachie ngazi ukweli ni kwamba Mwalimu alimshauri Kaunda asifanye uchaguzi kwa sababu taarifa za ki intelijensia alizokua nazo(na Mwalimu was good at that) zilionyesha Kaunda asingeshinda uchaguzi huo. Hayo ni maneno yake mwenyewe Nyerere na aliyatoa hadharani na kumbukumbu zipo

Kwa maneno mengine(hii ni tafsiri yangu) ni kama alikua anamwambia Kaunda awafanyie ubabe raia wake asifanye uchaguzi!!! Kama ikiwezekana aibe uchaguzi abakie kua Rais wa Zambia ushauri ambao Mzee Kaunda aliukataa, akaingia kwenye uchaguzi akiwa na tume huru kabisa kabisa kabisaaaa ya uchaguzi na matokeo yalipotangazwa aliyakubali bila kinyongo wala hila!

Hii ni legacy aliyoicha Mzee Kaunda ya ku set precedence ya kuheshimu demokrasia na kukubali matakwa ya raia na sauti yao kupitia sanduku la kura na kwa hilo Zambia wametushinda sana.

Kwa taarifa yako tu marehemu Mwalimu Nyerere ndiye alikua championi wa siasa za hila na ubabe wa kichama na ndio muasisi wa katiba tunayoilalamikia sasa na hata yeye mwenyewe baada ya kuachia ngazi kama rais lakini pia ndie fundi mkuu na injinia wa supremacy ya kibabe na ujanja ya Chama Cha Mapinduzi akidaiwa ndie aliyesimamia na ku set precedence ya kupindua matokeo ya chaguzi za Zanzibar (mbinu inayoigwa na Tanzania Bara pia) kwani hakutaka wala hakuamini chama au mtu asiyekua CCM aongoze Tanzania

Aliwahi tu wakati mmoja kumsifia Mandela kwamba ni bora kaondoka mapema madarakani kwani akisubiri azeeke akili inaweza kukataa kuondoka madaralani. Hapa kweli alikua anampiga vijembe Mugabe aliyekua amegoma kuachia wengine wagombee urais wa Zimbabwe

Tofauti yake na waliokuja kumrithi ni uwezo wake mkubwa wa kujenga hoja, akili angavu ya kuona mbali na hata uadilifu(hakuiibia nchi wala kua na double standards kwa wasaidizi wake). Kiasi kwamba mkono wake wa chuma haukuonekana wala hila zake hazikung'amuliwa mapema!

Pili ni suala la hali ngumu ya kiuchumi iliyoikumba nchi miaka ya mwanzoni ya 1980s hasa baada vita ya Kagera. Ni kweli yaliagizwa mahindi ya Yanga kutoka Marekani lakini si kweli kwamba yalitosheza na kwamba eti watu walikula na kusaza!!!

Kulikua na uhaba wa kila kitu ikiwemo bidhaa zote muhimu kama sukari, sabuni, mafuta ya kula na ya nishati n.k, ambapo zilipatikana kwa foleni na wakati mwingine kwa rushwa na hii ni kutokana na rigidity ya Mwalimu Nyerere kukataa kukubaliana na sera za mashrika ya fedha ya kimataifa na nchi wafadhili/wahisani
 
My Son drink water,
Kaunda aliondoka madarakani kupitia sanduku la kura halali, hakutumia polisi wala jeshi na hakulazimisha ushindi. Kaunda kura zilipohesabiwa na kutangazwa aliitikia na kupongeza, sijui unamsema Kaunda yupi mwingine.
 
ni kweli tunahitaji demokrasia ya ukweli na si ubabe na ujanja ujanja, haiwezekani toka mwaka 92 mpaka leo mwenyekiti wa CDM yupo tu madarakani na hataki kung'atuka. anabadili vipengele vya katiba ili afie madarakani. watanzania tukatae huu udikteta.
 
Kujiamini kwa Magufuli na kuwaambia waTanzania kwamba hato toa chakula kwa sehemu yoyote ya Tanzania itakayo kumbwa na baa la njaa, imesaidia Tanzania kuzalisha chakula kingi sana na kuongoza katika nchi za Afrika Mashariki, kati na kusini kwa miaka yote ya awamu ya tano. Ni legacy tosha.
 
Back
Top Bottom