Rais Magufuli abatilisha muda wa usajili wa laini za simu kwa kutumia Vitambulisho vya NIDA kama ilivyotangazwa awali na TCRA

Mimi sijaelewa

Zoezi lilipaswa kuanza 1st May mpaka Dec 31

Sasa Rais kasema Mwisho ni dec 31 hapo sasa Katengua nini?
 
NIDA na TCRA wapo sawa ila system walio itumia ya mtu kuomba namba yake ya kitambulisho cha NIDA ndo walibuma walitakiwa waweke free kwa watu kupata ID NO zao. Ndo maana itacheleweshwa usajili finger print
 
Sema mitandao yenyewe hawajitilia mkazo wa kuwaelimisha watanzania jinsi ya kupata ID NO ya NIDA yko utakayo tumia kusajili lain
 
Kulikua na haja gani ya kuweka ukomo juu ya hilo? wengine wapo njenya nchi sasa wakija wasipate mawasiliano? wengine bado hawajakua kwa hiyo wakikua hawatapata mawasiliano?

Nadhani wanatakiwa walitazame upya hilo jambo.
 
Naibu waziri juzi kasema bungeni kuwa zoezi linaanza tarehe 01/05/2019 mpaka December
 
Amesema watanzania wapo milion 55 lakini waliosajiliwa NIDA ni million 15 tu.

Hivyo tangazo la TCRA kuwa mwisho tarehe 1 mwezi wa tano itapelekea watanzania zaidi ya milioni 25 kukosa haki ya kumiliki mawasiliano.

Ameongeza muda mpaka tarehe 31 mwezi wa kumi na mbili, hata hivyo muda utakuwa mwisho endapo usajili wa vitambulisho utakuwa umekidhi vigezo.

Kama usajili haujakamilika watu waendelee kumiliki simu zao mpaka NIDA watakapokamilisha usajili wa vitambulisho.
Hujamwelewa.Hata TCRA walisema mwisho ni Dce 31 na Kenge Wa Lugola alifafanua hivyo bungeni. Rais kasema usajili wa laini kwa kitambulisho cha taifa uendane na usajili wa vitambulisho vya taifa na ifikapo dec 31 kama NIDA hawajakamilisha usajili basi usajili wa laini kutumia vitambulisho vya taifa utakuwa hauna maana.
 
Amesema watanzania wapo milion 55 lakini waliosajiliwa NIDA ni million 15 tu.

Hivyo tangazo la TCRA kuwa mwisho tarehe 1 mwezi wa tano itapelekea watanzania zaidi ya milioni 25 kukosa haki ya kumiliki mawasiliano.

Ameongeza muda mpaka tarehe 31 mwezi wa kumi na mbili, hata hivyo muda utakuwa mwisho endapo usajili wa vitambulisho utakuwa umekidhi vigezo.

Kama usajili haujakamilika watu waendelee kumiliki simu zao mpaka NIDA watakapokamilisha usajili wa vitambulisho.
His mbona TCRA walishatoa ufafanuzi Kuwa mwisho no December 2019?
 
Asema zoezi liendelee hadi december hapa naona huwa hakuna mawasiliano maana ni kutengua ili kupata credit
“Unaposema lazima watanzania wasajili laini za simu kwa kitambulisho cha taifa na wakati NIDA hawajamaliza kutoa vitambulisho kwa watanzania hii haiwezekani, lazima zoezi la kutoa vitambulisho liende na usajili”Rais Dkt.Magufuli ziarani Mbeya.
Watendaji wetu wana nidhamu ya yoga, haiwapi nafasi ya kuchemsha bongo zao. Mwingine boss wa TRA kasema mwisho wa pombe zisizo na sticker za electronic ni mwezi huu. Si waziri wa viwanda wala wa fedha, wote wako kimya, hata wa kusema wenye hizo chupa wanunue sticker, hakuna, wanamsubiri rais.
 
Mh! Mbona hili amelitolea ufafanuzi wa majibu haraka hivyo!

Vp Kuhusu habari za CAG na yule bwana sabufa ya milembe ndo kusema hazijamfikia ama dhalahu tu
 
lengo ni kuhakikisha by 2022 watanzania wote wana NIDA. ..bila hicho hutapata huduma yoyote
 
Amesema watanzania wapo milion 55 lakini waliosajiliwa NIDA ni million 15 tu.

Hivyo tangazo la TCRA kuwa mwisho tarehe 1 mwezi wa tano itapelekea watanzania zaidi ya milioni 25 kukosa haki ya kumiliki mawasiliano.

Ameongeza muda mpaka tarehe 31 mwezi wa kumi na mbili, hata hivyo muda utakuwa mwisho endapo usajili wa vitambulisho utakuwa umekidhi vigezo.

Kama usajili haujakamilika watu waendelee kumiliki simu zao mpaka NIDA watakapokamilisha usajili wa vitambulisho.
Mkuu, kwanza si kweli mwisho wa usajili ni trh 01/05/2019.hiyo ni tarehe ya kuanza usajili,mwezi wa 09 mwaka huu wa 2019 watahakiki idadi ya wasajiliwa,na mwezi wa 12 mwaka huu wa 2019 waziri alidai laini ambazo zitakua hazijasajiliwa mamlaka ya mawasiliano nchini watazima laini zisizo na usajili,

Tuanzie hapo na uzi ulioleta
 
Tundu lissu alipozungumza akaonekana bonge la mchochezi.
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔

Now yanazidi kutimia
 
Mkuu, kwanza si kweli mwisho wa usajili ni trh 01/05/2019.hiyo ni tarehe ya kuanza usajili,mwezi wa 09 mwaka huu wa 2019 watahakiki idadi ya wasajiliwa,na mwezi wa 12 mwaka huu wa 2019 waziri alidai laini ambazo zitakua hazijasajiliwa mamlaka ya mawasiliano nchini watazima laini zisizo na usajili,
Return kwani TCRA walisemaje, this is out of my sight please!
 
Back
Top Bottom