Rais Magufuli aamuru Ney wa Mitego aachiwe huru na wimbo wake upigwe vituo vyote redio na TV

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe, ameliagiza Jeshi la Polisi kumuachia huru Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego' aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi hilo.

Waziri Mwakyembe ameishauri pia BASATA kuondoa zuio lake dhidi ya wimbo huo, na badala yake uendelee kupigwa tu kama nyimbo nyingine.

Akiongea na Wandishi wa Habari muda huu mjini Dodoma, Dk. Mwakyembe amesema hata Rais Magufuli amefurahishwa na wimbo huo wa WAPO, na kumshauri Msanii huyo kama inawezekana aendelee kutaja watu wengine kama vile Wakwepa Kodi, Wauza Unga, Wabwia Unga, Wezi pamoja na watu wengine wasio na maadili mema katika jamii.







Nyimbo yenyewe ndio hii



MAONI YA MLETA UZI
Watanzania tumtumie Vizuri huyu Rais kkwa kweli hatakuja kutokea nani alifikiria hili.

Habari zaidi kuhusu huu Wimbo wa Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego' Soma;

Morogoro: Msanii Emmanuel Elibariki 'Nay wa Mitego', akamatwa na Polisi

BASATA: Wimbo wa WAPO wa Ney wa Mitego kufungiwa, hauna Maadili

BASATA: Marufuku kusikiliza au kusambaza nyimbo zilizopigwa marufuku
 
Back
Top Bottom