Rais Magufuli aahirisha sherehe za Mashujaa

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Rais Magufuli ameahirisha sherehe za mashujaa zilizopaswa kufanyika Julai 25, 2020, Jijini Dodoma na kuwataka Watanzania kuitumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwaombea mashujaa wote waliojitoa kwa ajili ya Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 18, 2020, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, na kuongeza kuwa Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano.

Aidha Rais Magufuli pia amewataka Watanzania kuwaombea Mashujaa wote hata wale ambao wametoa mchango mkubwa katika ngazi mbalimbali, ikiwemo kwa mtu mmoja mmoja ama familia.

1595056825400.jpeg
 
Hivi Rais wetu anapotutaka watanzania tuendelee kudunisha amani na utulivu......

Hivi anaelewa msingi mkubwa wa kudumisha amani na upendo?

Ni kwa nchi kutenda mambo yake kwa haki na usawa

Ajiulize hivi yeye anatekeleza "principle" hiyo Kuu ya amani?
 
1. Uzalendo nini?

2. Uzalendo unaanzia wapi? Asili na chanzo

3. Tunaweza kujifunza uzalendo namnagani

4. Zipi njia kuu za kuenzi uzalendo

5. Tunawalithisha vipi vijana na watoto uzalendo

Tunapofuta sherehe za wazalendo wa kweli-MASHUJAA watanzania waliojitoa kwa uhai, mali na kila kitu wakaifia nchi ..... tunathamini UZALENDO?
 
kuahirisha sherehe hizi ni kitu kizuri mno , hii ni staili ile ile ya kubana matumizi ya kipumbavu ya Nyerere!! Magu anapatia kwenye mambo mengi, mno, ni Rais bora kwa kubana matumizi, hawa mashujaa ni muhimu , uhuru ni muhimu, mapinduzi ni muhimu ila si lazima kufanya sherehe zake! hata vipindi vya television na redio vinatosha!!!

Magu ana shida tatu

1.Magu ni mdini, anateua wakristo watupu na bomu analotengeza nchini kuna siku litalipuka na hakutakuwa na kurudi nyuma!

2. Magu ni mtu muoga wa kukosolewa na kushindana na wengine ulingoni, anazuia demokrasia ndani ya sisiem na anazuia demokrasia ya vyama vingi isifanyike na katika utawala huu wapinzani wana shida zaidi , hivyo kuzalisha fikra za kudai tume huru , katiba mpya na utawala wa sheria

3.Wachumi wake Magu hawamwambii ukweli kuwa sera zote za uchumi za sasa zinajenga uchumi wa serikali na kubomoa kabisa maisha ya raia ambao wanamchukia sana moyoni ila kwakuwa wabongo wana hulka ya unafki hawasemi kwasasa yuko madarakani na kuna mabuti, virungu, maji ya washawasha na mabomu ya machozi!!

kuna mahali kwenye mada ya ajira ajira ajira nimeeleza kwa kina na lugha rafiki sera za uchumi za serikali hii zinazowafanya raia wote wasio na kazi serikalini na katika formal sector kuwa masikini wa kutupwa karibu 92% ya able bodied people!

lets us all tell our M/kiti openly ili arekebishe mapungufu yake ngwe ya pili ya lala salama awe bora zaidi maana tayari amethibitisha kwa vitendo kuwa yeye ni Rais mzalendo , mchapakazi na mkweli kuliko wote bongo.
 
Rais Magufuli ameahirisha sherehe za mashujaa zilizopaswa kufanyika Julai 25, 2020, Jijini Dodoma na kuwataka Watanzania kuitumia siku hiyo kuwakumbuka na kuwaombea mashujaa wote waliojitoa kwa ajili ya Tanzania.

Taarifa hiyo imetolewa leo Julai 18, 2020, na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, na kuongeza kuwa Rais Magufuli amewataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, upendo, utulivu na mshikamano.

Aidha Rais Magufuli pia amewataka Watanzania kuwaombea Mashujaa wote hata wale ambao wametoa mchango mkubwa katika ngazi mbalimbali, ikiwemo kwa mtu mmoja mmoja ama familia.

View attachment 1510030
CCM hakuna utulivu sasa na vuguvugu la chinichini linaendelea watu wamechoka.
 
kuahirisha sherehe hizi ni kitu kizuri mno , hii ni staili ile ile ya kubana matumizi ya kipumbavu ya Nyerere!! Magu anapatia kwenye mambo mengi, mno, ni Rais bora kwa kubana matumizi, hawa mashujaa ni muhimu , uhuru ni muhimu, mapinduzi ni muhimu ila si lazima kufanya sherehe zake! hata vipindi vya television na redio vinatosha!!!

Magu ana shida tatu

1.Magu ni mdini, anateua wakristo watupu na bomu analotengeza nchini kuna siku litalipuka na hakutakuwa na kurudi nyuma!

2. Magu ni mtu muoga wa kukosolewa na kushindana na wengine ulingoni, anazuia demokrasia ndani ya sisiem na anazuia demokrasia ya vyama vingi isifanyike na katika utawala huu wapinzani wana shida zaidi , hivyo kuzalisha fikra za kudai tume huru , katiba mpya na utawala wa sheria

3.Wachumi wake Magu hawamwambii ukweli kuwa sera zote za uchumi za sasa zinajenga uchumi wa serikali na kubomoa kabisa maisha ya raia ambao wanamchukia sana moyoni ila kwakuwa wabongo wana hulka ya unafki hawasemi kwasasa yuko madarakani na kuna mabuti, virungu, maji ya washawasha na mabomu ya machozi!!

kuna mahali kwenye mada ya ajira ajira ajira nimeeleza kwa kina na lugha rafiki sera za uchumi za serikali hii zinazowafanya raia wote wasio na kazi serikalini na katika formal sector kuwa masikini wa kutupwa karibu 92% ya able bodied people!

lets us all tell our M/kiti openly ili arekebishe mapungufu yake ngwe ya pili ya lala salama awe bora zaidi maana tayari amethibitisha kwa vitendo kuwa yeye ni Rais mzalendo , mchapakazi na mkweli kuliko wote bongo.
Umeeleza vizuri ila hapo kwenye udini umepuyanga mkuu
 
Back
Top Bottom