Rais Magufuli aagiza wastaafu Polisi kulipwa, asema wanaowacheleweshea haki ni wakubwa wao wanaokaa kwenye viyoyozi

Sisi watanzania bhana utendaji wetu ni wa kizembe mno, nendeni kwenye ofisi za serikali yaani mtu anaweza akazunguka na karatasi yako week nzima, mbaya zaidi hata kukupa taarifa kuwa tuko kwenye hatua hii au haiwezekani hawa wezi , lazima uwa tafute wewe mwenyewe, watendaji wetu ni wakusukuma hadi dakika za mwisho ndo wanafanya kazi.
 
Tatizo ni kwamba Rais amekumbatia fedha zote za umma na hivyo kusababisha baadhi ya taasisi zake kukosa ufanisi. Matumizi yo yote ya serikali lazima yapate idhini yake, na bahati mbaya sana idhini inatolewa katika kazi anazotaka au kuzipenda yeye.

Mafao ya wastaafu yanapaswa kulipwa mara moja bila kuanza kupiga kelele au kuomba kibali) idhini ya Rais. Taratibu za kisheria lazima zizingatiwe katika kulipa mafao ya wastaafu na wala siyo hisani ya Rais.
Hizo ni siasa!!kwani ni wastafu tu kutoka jeshi la polisi ndio hawajalipwa?!!mbona kila wizara hali ni hiyo hiyo tu!?tatizo ni pale mifumo inakuwa haifanyi kazi hadi mtu mmoja aamue!!na hapo utasikia baada ya wiki moja pesa imepatikana na wamelipwa!!yaani umaondoa tatizo ki zima moto!!utegemee kuwa litakwisha!!
 
'Nawashangaa Wizara ya mambo ya ndani. Una wastaafu, wamemaliza kazi ya Polisi bila tatizo, Waziri utakaa ofisini bila kwenda kuwaombea. Kwanini usichukue majina kwenda Wizara ya Fedha ukasema nina wastaafu nataka fedha.'...
Porojo hizo!!ina maana toka lini kazi ya kupeka majina ya wastafu inakuwa ya mawaziri?!!kila wizara inafahamu idadi ya wafanyakazi wake wanaokwenda kustafu.
 
Rais ama PM wanapopata platform ya ku-address tatizo ambalo lipo wizara zote ni vyema wakalitolea kauli kwa ujumla wake.

Sidhani kama hii issue ipo wizara ya Mambo ya ndani pekee.

Polisi watalipwa ndani ya hiyo wiki moja,Je wale wasio polisi na wanapitia shida hiyo inakuwaje?

Wasubiri tukio la wizara zao nao wakasome risala?
 
Taratibu za mafao ya watumishi zinaeleweka waziri, katibu au Igp si kweli wanahusika na hilo tatizo halipo polisi ni watumishi wengi wa umma wanaostaafu wanalalamika kuhusu mafao yao
 
Sio Mitano tena ni milele kabisa tafadhali.
Uchumi wa kati....
Nchi hii ni tajiri sana....
Au nasema uongo ndugu zanguuuuu....

Unayajua mavieitee wewe...
Sisi tunatembelea mavieitee...

Wakati wanaumuza wapinzani walitegemea nini???
Mimi naona wasilipwe kabisa maana mapolisi Ndio wamewaweka hao madarakani
 
Yaani ni matatizo makubwa kwa watendaji...anaweza kuamua kuwalipa akakaangwa..au akaamua auchune ukakaamgwa vilevile..

Hali ni ngumu kwa watendaji wetu, waoneeni huruma!!
Ila ukiwa pale lazima ubakie kimya na ulilie tumboni.
Kwa mawazo yangu nadhani suala la kuwalipa wastaafa ni process ambayo ilipaswa iwe rahisi na straight foward kabisa. Na pia inapokwama, viongozi kama rais kufuatilia na kujua ni nani anakwamisha na kumwajibisha ingepaswa kuwa rahisi sana. Hii ni kwa sababu ni kitu ambacho kina hatua zinazojulikana na hazitoi nafasi ya mizengwe. Hivyo nitakubaliana na wewe ni lazima kuna kitu ambacho kiko nje ya wanashughulikia malipo kinawakwamisha.
 
Mbona wastaafu wengi tu hawajalipwa pesa yao...au huyu jamaa wastaaf ni hao polos tu katika nchi hii?
Hili ndilo tatizo la uongozi wetu. Hawataki kushughulikia matatizo kwa ujumla na kwa kuweka mfumo. Mimi nilidhani hapo ndiyo ingekuwa nafasi ya kujua wastaafu wote ni kwa nini wanakwamishwa na kuondoa kona kona zote zilizopo na kama kuna uzembe kurekebisha.
 
Umpende, usimpende; kubaliana naye au mkatalie...Ila JPM ni mwanasiasa hasaa 😅

Amewakamata watendaji wote akawafunga kamba kama vikaragosi anawechezesha mdundiko wake. Amewafanya ukuta baina yake na wananchi kwa kutupiwa kila ovu au baya. Kila zuri atalipitisha kuja kwake. Amewafungia "milango na mageti ya kifikra" majirani na mataifa ya nje kwenye akili za watanzania wengi. Atafungua tu kama wanampa anachotaka na si vinginevyo.

Anajua anahitaji "mioyo" ya wananchi kwa yajayo na anawapanga ipasavyo. Ametumia, na ataendelea kutumia imani kama "mafuta ya kumpamba au kujinasua"... "anapigania" haki za "wanyonge" na kuwa balozi wao mkuu; kundi moja baada ya lingine. Akipata tu anachotaka, tutaona mabadiliko mapya.

Eneweiii...Mola atupe mwisho mwema na wenye heri tu maana Dunia hadaa, Ulimwengu shujaa.
 
Sijaamini hii kauli. Polisi walivyo na mishahara midogo na wanavyofanya kazi kwenye mazingira magumu , bado wakistaafu wanacheleweshewa kulipwa pensheni zao?
Tena mi napendelea wanyimwe kabisa. Rushwa walizochukua zinatosha kabisa
 
Back
Top Bottom