Rais Magufuli aagiza wafungwa waanze kufanya kazi za uzalishaji mali magerezani

T2015CCM

JF-Expert Member
Sep 13, 2012
7,931
987
ametoa agizo hilo katika hotuba yake akiwa katika ziara ya siku tatu mkoani pwani.amesema ni marufuku mfungwa kulala na kutoka gerezani akiwa na kitambi, wafanye kazi ngumu ili waogope kwenda kwenda huko, na wakienda huko gerezani wajifunze uchapakazi na pia wafanye kazi za uzalishaji mali. wailishe nchi sio wao ndio walishwe na watanzania.
 
Naunga mkono kauli ya Rais japo sio kwa nia ya ukomozi kama yake, bali nafikiri juu ya rehabilitation ya ndugu zetu waliokengeuka.

Huko magerezani kumejaa watu wazuri tu, ambao pengine wamefungwa sababu za kijinga tu kama kutukanana na jirani au kuiba kuku. Kule wanawekwa bila shughuli wala mwelekeo kwa jina la GEREZA na matokeo yake wakitoka huko wanakuwa maharimia wa kutupwa. Ukimfunga mtu wa miaka 23 kifungo cha miaka 6 basi juwa kuwa muda wake wa misuli moto ameumalizia idle akijiandaa kuja kufanya NOTHING baada ya kutoka huko.

Lakini mtu huyo huyo akipatiwa shughuli ya kufanya atatoka gerezani na ujuzi na akili njema. Mimi nakumbuka duka la magereza pale KEKO ndio lilikuwa supermarket yetu miaka ya 80 kwani maharage ya magereza yalikuwa yamechambuliwa kabisa.

Badala ya kununua bombadier, Mheshimiwa Rais anunue matrekta wapewe magereza watulimie chakula ili hatimaye serikali iache kupora mazao ya wakulima kwa kisingizio cha akiba ya chakula. Kwa hili Mheshimiwa Rais nitakuunga mkono na kukupeperushia bendera.

Wasipewe kazi ngumu as if tunawakomoa, wapewe kazi zalishi ili wajielewe kuwa wao ni wa muhimu na maana kwa taifa hili.
 
Yaani hapo naunga mkono. Wafungwa wanakaaje mjini??
Mfano magereza ya Iringa inakuwaje mjini bwana??
Kwa nini mfungwa aliyefanya kosa alishwe na mtu ambaye hajafanya kosa??
 
Hili swala naliunga mkono. ..hata ujenzi wa madarasa. ..ufyatuaji wa matofali kujenga shule hawa jamaa watusaidie
 
Rais atoe tamko la kuzuia unyama unaofanywa kwa lengo la kuwavunjia heshima hasa viongozi wa upinzani ambao wanakamatwa na kuwekwa ndani ovyo ovyo na wakuu wa mikoa na wilaya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom