Rais Magufuli aagiza wafugaji waliowachapa wananchi viboko wakamatwe

ng'ombo

JF-Expert Member
Dec 1, 2014
418
619
Screenshot_2017-03-17-22-33-42-1-1.png


Rais John Magufuli amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Alhaji Majid Mwanga kuwasaka, kuwakamata na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wafugaji wote wanaodaiwa kuhusika katika matukio ya kuwashambulia kwa viboko wananchi wa Kijiji cha Fukayosi kilichopo Wilayani humo.

Rais Magufuli aliyekuwa akisafiri kwa gari kutoka Dodoma kuja jijini Dar es Salaam ametoa agizo hilo leo aliposimama katika kijiji hicho baada ya kuona wananchi wengi wakiwa wamekusanyika kando ya Ofisi ya Kata.

Taarifa iliyoletwa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu, imeeleza kuwa baada ya kusimamisha msafara wake, Rais aliwaita wananchi waliokuwa wamekusanyika huku wakiwa wameshika mabango yaliyoandikwa ujumbe wa kutaka wafugaji wa jamii ya Wamang’ati waondolewe na kisha akatoa nafasi kwa baadhi yao kueleza dukuduku lao.

“Kuanzia leo isitokee mfugaji kumpiga mkulima, mkulima kumpiga mfugaji wala mfugaji kulisha mifugo yake kwenye mashamba ya wakulima, na suala hili nitalifuatilia mimi mwenyewe.

“Kwa hiyo Mkuu wa Wilaya na Viongozi mlishughulikie hili kabla mimi sijawashughulikia nyinyi, wale waliopiga watu, nataka wote wakamatwe na wafikishwe kwenye vyombo vya sheria” amesema Magufuli.

Source: Mwananchi
 
Ikiwa kama jambo hili linahitaji maelekezo toka juu, naanza kuwaamini wanasema jeshi LA MTU mmoja halitashinda vita.
 
Back
Top Bottom