Rais Magufuli aagiza Tsh. Bilioni 40 zitumike kulipa madeni ya Wakulima wa Korosho baada ya Serikali kununu Korosho hizo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Rais Magufuli ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kutoa Tsh. Bilioni 40 ili kumalizia madeni yote ya Wakulima wa Korosho yaliyobaki baada ya Serikali kununua korosho hao katika msimu wa mwaka 2018/19

Ametoa maagizo hayo leo alipokutana na viongozi wa Wizara, Mikoa, Wilaya na Taasisi za Serikali ambazo zinahusika katika uzalishaji wa mauzo ya zao la Korosho

Pamoja na kuagiza fedha hizo zitoke kesho Novemba 02, amewataka Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha fedha hio zinawafikia Wakulima na kuhakikisha wanaolipwa ni Wakulima wanaostahili

Aidha, ameelezea kutoridhishwa kwake na utendaji wa Wizara ya Kilimo na viongozi wa Mikoa na Wilaya ambapo katika maeneo yao kumetokea wizi mkubwa wa fedha za Wakulima kupitia Vyama vya Ushirika (AMCOS)

052E18F1-0076-4A63-939E-D272434D476F.jpeg

9E2EDBA1-FA82-4585-A08C-1B25472D0E38.jpeg
 
Rais Magufuli ameiagiza wizara ya fedha kutoa jumla ya sh 40 bilioni ili kumaliza madeni wanayodai wakulima wa korosho.

Kadhalika mh Rais Magufuli amesema bado hajaridhishwa na utendaji wa wizara ya kilimo kwani bado kuna dhulma na wizi wa fedha za wakulima kunakofanywa na vyama vya ushirika

Source ITV habari!
 
Kama kodi yangu inanunua Korosho, hizo Korosho zipo wapi mbona sizioni mtaani nizile ?, Kwanini kama bado zipo kwenye maghala hazijanunuliwa basi wazimwage mtaani kwa bei ya kiungwana watanzania wapate kubadilisha ladha...
 
Rais Magufuli ameiagiza wizara ya fedha kutoa jumla ya sh 40 bilioni ili kumaliza madeni wanayodai wakulima wa korosho.

Kadhalika mh Rais Magufuli amesema bado hajaridhishwa na utendaji wa wizara ya kilimo kwani bado kuna dhulma na wizi wa fedha za wakulima kunakofanywa na vyama vya ushirika

Source ITV habari!

Si alidai pesa zote zilikuwa zimetengwa kabisa kabla ya korosho kununuliwa na serikali kabla ya jeshi kupelekwa?
Bora kumuamini Kigogo kuliko jiwe.
 
Rais Magufuli ameiagiza wizara ya fedha kutoa jumla ya sh 40 bilioni ili kumaliza madeni wanayodai wakulima wa korosho.

Kadhalika mh Rais Magufuli amesema bado hajaridhishwa na utendaji wa wizara ya kilimo kwani bado kuna dhulma na wizi wa fedha za wakulima kunakofanywa na vyama vya ushirika

Source ITV habari!
Serikali ikome kujiinguza kwenye shughuli ambazo hakustahili. Yote haya kaharibu Meko, amekuta wadau wa korosho wameanzisha mfuko wa maendeleo wa zao la Korosho. Mfuko ulikuwa unasimamiwa na Bodi ya Korosho, alipoingia akavunja Bodi na kuchukua hela za mfuko na kuziingiza kwenye mfuko wa hazina. Walimuonya bungeni lakini hakushaurika na akaishia kusema eti wanasiasa wana uchezea mfuko wa korosho.

Kama angekuwa ameacha korosho iendelee kusimamiwa kama ilivyokuwa zamani basi mfuko huo ungesaidia kufidia wakulima pale bei ya Korosho inapokuwa imeteremka kama mwaka huu.

Lakini vichwa vya Watanzania vimejaa kamasi tu, utasikia wanamshangilia kwa hii taarifa ya leo.
 
Back
Top Bottom