Mgambilwa ni mntu
JF-Expert Member
- May 30, 2017
- 2,869
- 3,188
Kufuatia kuisha tarehe 16.06.2018 kwa muda wa Mwezi mmoja uliotolewa Mwezi Mei 17, 2018 na Rais John Pombe Magufuli akiwa katika hafla ya Uzinduzi wa Kituo cha Uwekezaji cha Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kupitia Suma JKT, sasa Suma JKT wametoa orodha ya wadaiwa wa matrekta 1,561 na kupewa go ahead ya kuanza kuwakamata wadaiwa hao kuanzia Jumatatu ya tarehe 16.07.2018.
Orodha hiyo ina Vigogo kadhaa wakiwemo Mawaziri, Mawaziri Wastaafu, Wabunge, pamoja na Wakuu wa Mikoa. Mojawapo ya Majina maarufu ni: Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo.
Kwa kuwa, Lugola ndiye bosi wa majeshi yaliyopewa mandate ya kukamata, anapaswa kuwa wa kwanza kulipa deni hilo ili lisije kuathiri utendaji wake lakini zaidi lisiathiri utendaji kazi wa Polisi katika kuwatia nguvuni wadaiwa.