Rais Magufuli aagiza RCO Morogoro kusimamishwa kazi, malipo ni hapa hapa.

Na Malisa GJ.

Uliwahi kuona asubuhi kuku anakula mchele wa kupika biriani, halafu jioni analiwa kwenye biriani hilohilo. Ni hiki kilichomtokea RCO Moro. Juzi aliwakamata Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa Patrick Ole Sosopi na mgombea ubunge Kwela Daniel Naftal Ngogo wakiwa Ifakara kwa madai kuwa wameanza kampeni kabla ya muda.

Kesho yake akawakamata viongozi wa Chadema waliokuwa wameweka kambi Morogoro mjini akiwemo diwani Gisunte Nice.

RCO huyo wiki iliyopita aliagiza viongozi wote wa Chadema waliokua Mlimba, ambao si wakazi wa Mlimba wakamatwe. Wakavamiwa na kukamatwa, na kuwekwa rumande kituo cha polisi Ifakara.

Jana asubuhi Mdude Chadema alimtumia ujumbe akimuonya kwamba roho mbaya haijengi. Mdude alimwambia RCO kwamba Chadema inaweza kumshtaki, na akipatikana na hatia atapaswa kuwalipa wote aliowasababishia usumbufu. Hata kama atakua amestaafu, tutagawana pensheni yake.

Baada ya Mdude kuongea hivyo, RCO akatuma askari kwenda kuwakamata viongozi wa Chadema wilaya ya Kilosa waliokua wameenda Morogoro mjini kwenye kikao. Akasema wanafanya siasa nje ya wilaya yao kinyume na agizo la Rais kwamba kila mtu afanye siasa kwenye eneo lake. Baadhi ya viongozi wakakamatwa na wengine wakafanikiwa kuponyoka akiwemo kamanda David Chiduo.

Baada ya kukamilisha kuwasweka ndani viongozi hao, akiamini amemfurahisha Rais JPM, mara akakutana na taarifa kuwa JPM ameagiza asimamishwe kazi.

Kumbuka amesimamishwa kazi, sio kushushwa cheo. Yani kuanzia jana huyu sio mtumishi tena wa jeshi la polisi hadi uchungzi wa kuwanyanyasa wafanyakazi wa kiwanda cha Tumbaku utakapokamilika.

Hana tena zile nyota zilizokua zinampa kiburi. Hana tena sauti ya kuagiza fulani akamatwe. Hana tena gari lenye king'ora. Hana tena mamlaka ya kumpa amri mtu yoyote zaidi ya watoto wake. Tunakutana nae mtaani kama raia wa kawaida. That is power of karma. What goes arround comes arround.!
 
Rais John Magufuli amemuagiza katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Ndani, kumsimamisha kazi mara moja RCO wa Mkoa wa Morogoro kutokana na kushindwa kushughulikia kesi ya unyanyaswaji wa watumishi wa kampuni ya Tumbaku Morogoro.

Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro linaongoza kwa kunyanyasa na kubambikizia watu kesi wakiwepo wafanyabiashara, viongozi wa vyama vya upinzani, wakulima, wafugaji na wananchi wa kawaida.

Ni jana tu huyu RCO aliwanyima dhamana viongozi wa BAVICHA leo yupo kijiweni, nasema malipo ni hapa hapa.


Umeona jinsi Mh. Rais wetu ni mtu wa haki kwa wote.. Hachagui dini, kabila wala chama.. Ila hapo hata kusema asante tu hujasema.
 
Unafurahia binadamu kupata matatizo!!

Hawa mapoliccm hayana akili kila uchao yanasemwa kwa kutotenda itakiwavyo bado yanaendelea kuisifu ccm na kutekeleza matakwa yao mwisho yanatumbuliwa yanakuwa hayana ndg wala rafiki.They have to think twice about ccm na mapanya buku yake.
 
Sahv RCO huyo atakuwa anangalia mchezo wa draft tu
Maisha mzunguko
Hayana formula

Ova
 
Morogoro ukituhumiwa ukafikishwa kituo cha polisi wale wapelelezi wanachukua simu yako kwanza wanaangalia kama Luna miamala iliyonona.wakikuta unajiweza wanachofanya ni kukuweka ndani mahabusu hata kama kosa lina dhamana hutoki mpaka umetoa pesa
hii hatari kabisa
 
Kwahiyo Jiwe ndio kamtumbua ,Kwenye hilo la kiwanda si alikuwa anatekeleza maagizo toka juu? Juu si kwa jiwe au nani mwingine .Katolewa kafala huyo .
 
RCO wa Tabora ajiandae. Wazungu wa JTI wanabambikiza makosa kwa wafanyakazi, polisi wanawatesa na kuwalazimisha wakiri, kuna mzee wamemvunja mbavu. Ngoja tuendelee kukusanya data...
 
Rais John Magufuli amemuagiza katibu Mkuu wizara ya Mambo ya Ndani, kumsimamisha kazi mara moja RCO wa Mkoa wa Morogoro kutokana na kushindwa kushughulikia kesi ya unyanyaswaji wa watumishi wa kampuni ya Tumbaku Morogoro.

Jeshi la polisi Mkoa wa Morogoro linaongoza kwa kunyanyasa na kubambikizia watu kesi wakiwepo wafanyabiashara, viongozi wa vyama vya upinzani, wakulima, wafugaji na wananchi wa kawaida.

Ni jana tu huyu RCO aliwanyima dhamana viongozi wa BAVICHA leo yupo kijiweni, nasema malipo ni hapa hapa.
Mimi nilitarajia Rais amwajibishe IGP halafu mengine yafuate mkondo.
 
Back
Top Bottom