johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,777
- 141,646
Rais Magufuli amemwamuru mkuu wa wilaya ya Nkasi pamoja na mkuu wa polisi wa wilaya hiyo kumlipa mama mjane jumla ya sh milioni 15 ikiwa ni thamani ya ng'ombe zake alizoibiwa.
DC na OCD walizembea na kusababisha mwizi wa ng'ombe kutoroka ilhali alishakamatwa na kufikishwa polisi.
Rais Magufuli amewapa siku 5 kulipa deni hilo.
Chanzo: TBC!
******
Rais Magufuli ameagiza Polisi wakiongozwa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo, Mathias Nyange na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Said Mtanda kumlipa Felista Mkombo Tsh. Milioni 15
Fedha hizo ni kama fidia kutokana na Polisi kutoshughulikia vizuri suala lake la kuibiwa ng’ombe ambapo mama huyo aliibiwa ng’ombe 25 na Polisi walimwachia Mtuhumiwa na baadaye Mtuhumiwa huyo akatoroka
Aidha, amesikitishwa na namna viongozi wa Mkoa huo wanavyoshughulikia kero za Wananchi na mara baada ya hotuba yake aliagiza viongozi hao wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Joachim Wangabo kubaki mkutanoni na kusikiliza kero za Wananchi waliokuwa wamebeba mabango