Rais Magufuli aagiza kufutwa kwa utitiri wa kodi

comrade igwe

JF-Expert Member
Jan 12, 2015
7,315
2,000
Wana JF salaam,

Rais wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa, Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri kuondoa utitiri wa kodi uliopo kwenye Mazao ili wakulima waweze kunufaika kutokana na kujiongezea kipato.Rais Magufuli akihutubia wakazi wa Kagera

Agizo hilo alimetolewa leo wakati akihutubia wakazi wa Wilaya ya Bukoba na watanzania kwa ujumla akiwa katika ziara ya kikazi ya siku mbili Mkoani Kagera.

“Nawaagiza Wakuu wa Mikoa,Wilaya pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri kupitia upya Kodi zilizopo katika bidhaa mbalimbali kama Kahawa na Pamba, hakikisheni mnaondoa utitiri huu wa Kodi ili wafanyabiashara hawa wafaidike na mazao yao,” Alisema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli amewaahidi watanzania kuwa atahakikisha anafanya kazi usiku na mchana bila kujali itikadi, dini na makabila ili kuhakikisha nchi inasonga mbele katika nyanja zote za kimaendeleo.

Akizungumzia maendeleo ya michango mbalimbali kwa ajili ya wathirika wa tetemeko la Ardhi mkoani Kagera Rais Magufuli amesema kuwa mpaka sasa simenti iliyochangwa ni zaidi ya tani 30,600 na mabati zaidi ya elfu 31,000 ambapo wananchi wameshaanza kupewa na kujengea.

Amewahimiza wananchi walioathirika na tetemeko la Ardhi kutotegemea Serikali kuwafanyia kila kitu na badala yake waanze kujenga na watumie msimu huu wa mvua kulima ili kujipatia chakula.

Pia Rais Magufuli amewashukuru na kuwapongeza wahisani waliochangia Maafa ya Kagera na kuwataka kuendelea na moyo huo katika kulijenga Taifa letu.

Chanzo: EATV
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom