Rais Magufuli aadhimisha sherehe za miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Jiji la Dodoma

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,491
54,884
Leo Watanzania kutoka nchi mbili za Zanzibar na Tanzania Bara wanaungano kusherehekea miaka 54 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulioasisiwa April 26, 1964
-
Lakini Muungano huu bado una kero ambazo hazijatafutiwa ufumbuzi licha ya kuwepo mijadala mbalimbali iliyolenga kuinua na kuimarisha Muungano
-
Changamoto(kero) mojawapo ni Hati ya Muungano ambayo inasimama kama Katiba ya Muungano ambayo bado inaleta changamoto katika uimarishaji wa Jamhuri.
-
Prof. Sherrif anaeleza kuwa, katika Hati ya Muungano, kitu kilichofanyika ni kwamba, jina la Serikali ya Tanganyika likabadilishwa na kupewa jina la Muungano wa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar
-
Anaeleza kuwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ipo lakini madaraka 11 ya serikali hiyo yalihamishwa na kupelekwa kwenye Serikali ya Muungano
-
Akahoji kuwa kwasasa tukiweka serikali 2 hizi katika mizani, zitakuwa hazina usawa tena, kwa sababu Serikali ya Muungano sasa imekusanya madaraka yote ya Tanganyika na mambo 11 ya Zanzibar

======

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameupandisha hadhi Mji wa Dodoma kutoka Halmashauri ya Manispaa na kuwa Halmashauri ya Jiji, na amemteua aliyekuwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Bw. Godwin Kunambi kuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli ametangaza uamuzi huo tarehe 26 Aprili, 2018 wakati akihutubia katika sherehe za kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma.

Pamoja na kuupandisha hadhi Mji wa Dodoma Mhe. Rais Magufuli ameagiza taratibu za kisheria zifanyike kukamilisha mchakato huo, na amesisitiza kuwa azma ya Serikali kuhamia Dodoma inaendelea kutekelezwa na kwamba yeye mwenyewe atahamia Dodoma mwaka huu.

Sherehe hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, Mke wa Rais Mhe. Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Seif Ali Idd na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa.

Viongozi wengine ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Ibrahim Hamis Juma, Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar Mhe. Omar Othman Makungu na Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu Mhe. Benjamin William Mkapa.

Katika sherehe hizo zilizohudhuriwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina, Mhe. Rais Magufuli ameishukuru AfDB kwa ufadhili wa miradi ya maendeleo yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 3.457 sawa na Shilingi Trilioni 7 na Bilioni 778 za Tanzania zikiwemo fedha za miradi 25 zilizotolewa kuanzia mwezi Novemba, 2017 yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.986 sawa na Shilingi Trilioni 4 na Bilioni 467 za Kitanzania.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza Watanzania wote kwa kutimiza miaka 54 ya muungano na amesisitiza kuwa yeye na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein wapo imara na wataendelea kuwa imara kuulinda na kuudumisha muungano, kuilinda amani na kupigania maendeleo ya Tanzania.

“Taifa letu linakwenda vizuri, uchumi wetu unakua vizuri, mwaka jana umekuwa kwa wastani wa asilimia 7 na mwaka huu tunatarajia utakua kwa wastani wa asilimia 7.1, mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa asilimia 4” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Kabla ya kuhutubia wananchi Mhe. Rais Magufuli amekagua gwaride rasmi lililoandaliwa na majeshi ya ulinzi na usalama na amewaongoza viongozi mbalimbali na wananchi kushuhudia maonesho ya gwaride, mazoezi ya kujihami, halaiki, muziki wa dansi na ngoma za makabila mbalimbali zilizotumbuiza uwanjani hapo.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amefanya mazungumzo rasmi na Rais wa AfDB Dkt. Adesina yaliyofanyika katika Ikulu ndogo ya Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na Rais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Shein.

Baada ya Mazungumzo hayo Dkt. Adesina amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya kuimarisha uchumi wa Tanzania na amesema wamejadiliana mambo kadhaa yakiwemo namna benki hiyo ilivyosaidia juhudi za maendeleo za Tanzania tangu mwaka 1971 na inavyoendelea kusaidia katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Ametaja baadhi ya maeneo ambayo AfDB itatoa ufadhili kuwa ni uzalishaji na usambazaji wa nishati, uboreshaji wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya Jiji la Dodoma hasa barabara.

“Yote kwa yote nimemhakikishia Mhe. Rais Magufuli kuwa AfDB itamuunga mkono katika mipango yake na maono yake ili tuweze kuisaidia Tanzania kukua zaidi, nimefurahi kuzungumza na Mhe. Rais na naona Tanzania ipo katika njia sahihi” amesema Dkt. Adesina.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dodoma

26 Aprili, 2018
 
Mkataba wa Muungano ulitiwa saini na Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, Aprili 22, 1964, Zanzibar.

Ulithibitishwa na Bunge la Tanganyika na Baraza la Mapinduzi Aprili 26, 1964, na Aprili 27, 1964 viongozi hao walikutana katika ukumbi wa Karimjee, jijini Dar es Dalaam kubadilishana hati za Muungano.

Sheria za Muungano ilitamka kwamba, Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar zililazimika, kuwa dola ya Jamhuri kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, jina ambalo lilibadilishwa Oktoba 28, 1964 na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupitia sheria ya Jamhuri ya Muungano, sheria namba 61, ya mwaka 1964.

Msingi wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984 ni Hati za Muungano za Mwaka 1964.
Hati za Muungano zilitiwa saini na Nyerere na Karume, Aprili 22, 1964 na hapo Tanganyika na Zanzibar kuwa dola moja kwa misngi inayotambulika kimataifa. Baada ya kuungana, Mwalimu Nyerere alikuwa rais wa kwanza na Karume alikuwa makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aprili 26, 1964, bunge la Tanganyika lilipitisha sheria za Muungano, ambazo baadayezilithibitishwa na Baraza la Mapinduzi Zanzibar.
Mnamo Aprili 27, 1964 waasisi wa Muungano walibadilishana Hati za Muungano na wajumbe saba wa Baraza la Mapinduzi waliapishwa kuwa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Watanganyika na Zanzibar ambao ni Amani Karume, Kassim Abdallah Hanga, Abdulrahman Babu, Hassan Nassor Moyo, Aboud Jumbe, Hasnu Makame na Idris Abdul Wakil. Kati yao, Aboud Jumbe na Hassan Nassor Moyo wangali hai.

Katiba ya muda ya mwaka 1965 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianisha mambo 11 ambayo yalikubalika kuwa ni ya Muungano ambayo ni; Katiba na Serikali ya Muungano, Mambo ya nchi za nje, Ulinzi, Polisi, Mamlaka juu ya mambo yanayohusika na hali ya hatari, Uraia, Uhamiaji, Mikopo na Biashara za nje, Utumishi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano, Kodi ya Mapato inayolipwa na watu binafsi na mashirika, ushuru wa forodha na ushuru wa bidhaa zinazotengenezwa Tanzania unaosimamiwa na idara ya forodha, Bandari, mambo yanayohusika na usafiri wa anga, posta na simu.

Katiba ya muda ya mwaka 1965 ilianisha utawala wa serikali ya mfumo wa chama kimoja, TANU kwa Bara na ASP kwa Zanzibar. Katiba hii, ilizingatia misingi ya makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 na sheria za Muungano wa Tangayika za Zanzibar.
Katiba hiyo ilianisha serikali mbili, uwakilishi wa Zanzibar katika bunge la Muungano ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano na mambo yasiyo ya Muungano kwa upande wa Tanganyika. Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikiwa na mamlaka juu ya mambo yote yasiyo ya Muungano yahusuyo Zanzibar.

Hata hivyo mambo ya Muungano yaliongezwa kutoka 11 hadi 22 kutokana na mahitaji ya ndani ya nchi pamoja na mabadiliko yaliyokuwa yanaendelea kutokea ulimwengini baada ya Muungano.

Mwaka 1985, jambo la 12 linalohusu sarafu na fedha kwa ajili ya malipo na kurahisisha usimamizi wa fedha za kigeni na benki katika Jamhuri ya Muunagno wa Tanzania, liliingizwa.

Kufuatia kuundwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1967, mambo matatu ya Muungano yaliyongezwa, ambayo ni leseni za viwanda na takwimu; elimu ya juu; na usafirishaji wa anga.

Mwaka 1968, mambo ya maliasili ya mafuta, pamoja na mafuta yasiyochujwa ya magari na ama ya petroli na aina nyingine za mafuta au bidhaa na gesi asilia yaliyongezwa kwenye orodha hiyo.

Aidha mambo ya Muungano yaliendelea kuongezeka hadi kufikia 21 kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mwaka 1992 kufuatia mabadiliko ya mfumo wa siasa nchini suala la 22 la uandikishaji wa vyama vya siasa na mambo mengine yanayohusiana navyo liliongezwa kwenye orodha hiyo.

MJADALA KUHUSU MUUNGANO
Katika miaka hivi karibuni kumekuwa na mijadala mbalimbali kuhusiana na muundo wa Muungano, baadhi wakitaka uwe wa zaidi ya serikali mbili, wengine serikali moja, wapo wanaotaka Tanganyika iwe kivyake na Zanzibar kivyake.
Hata hivyo hekima inaonyesha kwamba Muungano wa Tanganyika na Zanzibar unabaki kuwa ni fahari ya Watanzania, kwani mwelekeo wa dunia katika nyanja mbalimbali, mataifa kuungana kwa ushirikiano wa aina mbalimbali ni muhimu kuliko taifa moja kupambana kivyake.

Urejeaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kuvunjika mwaka 1977, uwepo wa SADC, ECOWAS, COMESA, na jumuiya nyingine nyingi duniani kote, ni vielelezo kwamba ushirikiano baina ya mataifa ni suala lisilohitaji mjadala.

Ieleweke kwamba hakuna ushirikiano usio kuwa na matatizo kama ilivyo kwa Muungano wa Tanzania, vivyo hivyo muungano mwingine kama vile ya United Kingdom (UK), Uingereza na United States of America (USA) kwa maana ya Marekani na United Arabs Emirate (UAE), nayo ina matatizo, lakini hata mara moja mjadala juu ya matatizo hayo siyo kuvunja ushirikiano bali kutatua na wale wanaotaka kuvunja hushughulikiwa ipasavyo.

"Matatizo ya Muungano kama wa UK ni mabaya zaidi, na hata UAE hawana ahueni, ila wanajua kwamba Muungano wao ni lazima. Wamarekani wanapambana na watu wenye mawazo haya ya kuvunja miungano kwenye majimbo ya Alaska, Hawaii na Texas na mwishowe wameamua kuweka kambi kubwa ya jeshi la nchi kavu Texas; utitiri wa kambi za anga Alaska; na vituo vikubwa kupindukia vya majini kule Hawaii. Hivi, hawa mabingwa wa demokrasia wanapoamua kulinda nchi yao namna hii, unafikiri ni wajinga?

Walimwaga damu na waliyanunua majimbo haya na wamepitia shida kubwa, ndiyo maana leo wanajidai," anaandika mchangiaji katika mjadala kuhusu Muungano.
Ni vyema Watanzania wakati huu wa kusheherekea miaka 54 ya Muungano, kila mmoja akajisikia ufahari wa kuwa na kitu kizuri kilichoasisiwa na Waafrika wenyewe na kudumu kwa umri huo.

Mawazo ya kubaguana kwa sababu zisizo na msingi, pengine kukidhi matakwa na wakati kama vile ya kibinafsi na kisiasa, yasipewe nafasi kuisambaratisha nchi. Chambilecho wahenga, umoja ni nguvu utengano ni udhaifu.
 
Tangu serikali ya awamu ya tano kuamua kuhamishia rasmi makao yake ktk mkoa wa Dodoma kumekuwa na mwamko mkubwa wa uwekezaji na wafanyabiashara kuwekeza ktk mkoa huo ambao jana umeteuliwa kuwa jiji, ni fursa adimu kwa wakazi wa jiji la Dodoma kuchangamkia fursa hizo za uwekezaji. Sio tu wakazi wa mji huo watanufaika bali hata mikoa jirani inayopakana na Dodoma hasa ya kanda ya kati nayo itanufaika, mikoa kama singida, Tabora nk ambayo inakaribiana na jiji hilo ni wakati muhafaka kuchangamkia fursa hizo. Kila lakheri ya mafanikio jiji la Dodoma.
 
Mie huo ukaribu wa Singida na Dodoma siuonagi, maana ni mbali sana.Sema Dodoma yenyewe ndio itafaidika lakini kwa mikoa mingine sioni hio kitu. Morogoro ni karibu zaidi na Dodoma kuliko Singida labda itafaidika zaidi.
 
Rais mwaka jana kwenye sherehe amesema "Atakae jaribu kuvunja Muungano atakiona" mwaka huu.
"Atakae jaribu kuvunja Muungano atakiona"

Hebu wekeni hapa nani anamtisha huyu mtu akawa kila mara hajiamini ana hofu?

Kauli zake ni za ovyo sana woga umemzidi anatumia vitisho tu hotuba zake.
 
Back
Top Bottom