Rais Magufuli aache siasa chonganishi. Mbunge gani wa CHADEMA alimuomba amteue?

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
23,341
55,133
Rais Magufuli tangu aingie madarakani amekuwa akitoa kauli za kuvunja undugu, umoja na utangamano kati ya wafuasi wa vyama vya siasa vya upinzani na chama tawala. Kwake yeye siasa ni uhasama. Na kama rais amelitilia mkazo sana suala hili.

Tanzania na dunia yote inajua kuwa:-
1. Alimdhalilisha Abdallah Bulembo mbele ya wanaccm wenzake kuwa amkanye binti yake ambaye ni mtu mzima kwa sasa (23) na ni mbunge, eti aache kutoka kimapenzi na mbunge wa upinzani. Anatoa siri za chama.

2. Kuna wakuu wa mikoa 2 wawili, mmoja alitumbuliwa na mwingine kulazimishwa kujiuzulu kwasabb tu walikuwa wakifanya kazi kwa mashirikiano mazuri na wapinzani.

3. Hâta Lowassa kisha lisemea hili mara nyingi tu, kuwa kuna wafanyabiashara wengi tu waliounga mkono upinzani 2015 wanashughulikiwa kwa mgongo wa kukwepa kodi na kulazimika kufunga biashara zao.

4. Kuna watumishi wametumbuliwa kwa hisia tu kwamba waliunga mkono upinzani 2015.

5. Hata ndani ya chama chake ccm amekuwa na mtazamo hasi dhidi ya waliokuwa wakiwaunga mkono wagombea wenzake 2015

Jamani iko mifano mingi sana ya kuchonganisha na kukomoa wapinzani wa kivyama na kifikra. Kwa ufupi JPM bado anaumwa ugonjwa wa "waliokuwa hawamuungi mkono 2015 nje na ndani ya chama"

Sasa jana, kwa makusudi kabisa baada ya kumuapisha yule mama wa ACT alitamka eti "kuna wabunge wa chadema wanamuomba awateue ". Rais Magufuli huu ni uchonganishi wa wazi kabisa. Ili kuwafarakanisha wabunge wa chadema, badala ya kujadili udikteta wako waanze kutafutana wao kwa wao. Tumekustukia, hatudanganyiki na wewe tunakuchukulia kama mzandiki tu.

Kama ni kweli weka hadharani jina na mawasiliano ya hao wabunge. Maana tunajua mawasiliano baina yako na mtu mwingine yeyote hunaswa na kuhifadhiwa.

Vinginevyo wewe kama raia namba moja nadiriki kusema umeshindwa kuwaunganisha watanzania na kuwaletea maendeleo. Badala yake umejikita kuvuruga vyama vya upinzani tu na kuwasulubu wale wote wenye mitazamo tofauti na wewe ndani ya chama chako. Hujiamini kabisa. Na umekosa dira.

Kama unajiamini ruhusu shughuli za vyama vya siasa zifanyike ! Ruhusu bunge live, ili wananchi waisikie bajeti yako na utekelezaji wake.

Ninakerwa sana na kauli zako vuruganishi.
 
Muongo sana huyu. Tangu aingie Ikulu nadhani hakuna hata Mbunge mmoja wa Chadema aliyekanyaga Ikulu kwa chuki zake za kutisha dhidi ya Chadema. Je, hao waliomuomba vyeo walimuandikia emails, text messages, kumpigia simu au kutuma ujumbe kupitia kwa wapambe wake? Kama kaamua kusema hili hadharani kwanini asiwataje Wabunge husika na kuweka ushahidi wa kutosha hadharani?
 
Ndiyo hapo mkuu, natilia mkazo kuwa mtu apingwe hadharani. Kimya cha wanachadema juu ya dhihaka hii kitachukuliwa kama ni kweli. Huu ni uzandiki
 
Yaani huyu mtu sijawahi kumpenda. Na anayoyafanya yanazidi kunichefua roho yangu. Simpendi na namchukia. Anataka watu wawachukie upinzani utadhani yeye anayoyafanya mazuri..ananikera sanaaaaa
Mnafki asie na namba,Hata namba moja haimtoshi.
 
Rais Magufuli tangu aingie madarakani amekuwa akitoa kauli za kuvunja undugu, umoja na utangamano kati ya wafuasi wa vyama vya siasa vya upinzani na chama tawala. Kwake yeye siasa ni uhasama. Na kama rais amelitilia mkazo sana suala hili.

Tanzania na dunia yote inajua kuwa:-
1. Alimdhalilisha Abdallah Bulembo mbele ya wanaccm wenzake kuwa amkanye binti yake ambaye ni mtu mzima kwa sasa (23) na ni mbunge, eti aache kutoka kimapenzi na mbunge wa upinzani. Anatoa siri za chama.

2. Kuna wakuu wa mikoa 2 wawili, mmoja alitumbuliwa na mwingine kulazimishwa kujiuzulu kwasabb tu walikuwa wakifanya kazi kwa mashirikiano mazuri na wapinzani.

3. Hâta Lowassa kisha lisemea hili mara nyingi tu, kuwa kuna wafanyabiashara wengi tu waliounga mkono upinzani 2015 wanashughulikiwa kwa mgongo wa kukwepa kodi na kulazimika kufunga biashara zao.

4. Kuna watumishi wametumbuliwa kwa hisia tu kwamba waliunga mkono upinzani 2015.

5. Hata ndani ya chama chake ccm amekuwa na mtazamo hasi dhidi ya waliokuwa wakiwaunga mkono wagombea wenzake 2015

Jamani iko mifano mingi sana ya kuchonganisha na kukomoa wapinzani wa kivyama na kifikra. Kwa ufupi JPM bado anaumwa ugonjwa wa "waliokuwa hawamuungi mkono 2015 nje na ndani ya chama"

Sasa jana, kwa makusudi kabisa baada ya kumuapisha yule mama wa ACT alitamka eti "kuna wabunge wa chadema wanamuomba awateue ". Rais Magufuli huu ni uchonganishi wa wazi kabisa. Ili kuwafarakanisha wabunge wa chadema, badala ya kujadili udikteta wako waanze kutafutana wao kwa wao. Tumekustukia, hatudanganyiki na wewe tunakuchukulia kama mzandiki tu.

Kama ni kweli weka hadharani jina na mawasiliano ya hao wabunge. Maana tunajua mawasiliano baina yako na mtu mwingine yeyote hunaswa na kuhifadhiwa.

Vinginevyo wewe kama raia namba moja nadiriki kusema umeshindwa kuwaunganisha watanzania na kuwaletea maendeleo. Badala yake umejikita kuvuruga vyama vya upinzani tu na kuwasulubu wale wote wenye mitazamo tofauti na wewe ndani ya chama chako. Hujiamini kabisa. Na umekosa dira.

Kama unajiamini ruhusu shughuli za vyama vya siasa zifanyike ! Ruhusu bunge live, ili wananchi waisikie bajeti yako na utekelezaji wake.

Ninakerwa sana na kauli vuruganishi.

Kama kuna mtu yeyote ndani ya CHADEMA alimuamini huyu jamaa basi huyo aliyemuamini naye anashida zake binafsi
 
Mm naamini hakuna. Mtu mwenyewe yuko very un-approachable.Unamuanzaje ?
 
Muongo sana huyu. Tangu aingie Ikulu nadhani hakuna hata Mbunge mmoja wa Chadema aliyekanyaga Ikulu kwa chuki zake za kutisha dhidi ya Chadema. Je, hao waliomuomba vyeo walimuandikia emails, text messages, kumpigia simu au kutuma ujumbe kupitia kwa wapambe wake? Kama kaamua kusema hili hadharani kwanini asiwataje Wabunge husika na kuweka ushahidi wa kutosha hadharani?
Akiba ya maneno inaitajika
 
Back
Top Bottom