Uchaguzi 2020 Rais Magufuli 28/10 tutakupa kura. Kama haya hayatafanyiwa kazi tutakutana tena 2025

Pagan Amum

JF-Expert Member
Aug 28, 2015
1,932
4,395
Kampeni za Lisu zimekushtua na zimeishutua CCM kuwa wananchi wengi hawakuridhika na namna ulivyoongoza katika kipindi hiki cha awamu ya kwanza. Tumekaa na kufikiria tumeona tukupe kura as the last warning kwa CCM. Kama haya hayatafanyiwa kazi basi 2025 CCM isihangaike hata kuweka mgombea.

1. Ajira kwa vijana. Sio uajiri tu walimu na madaktari. Kumbuka kuna kada lukuki vyuo vinazalisha kila mwaka

2. Kufufua private sectors na kuacha kuua private sectors tena

3. Kupandisha mishahara kwa watumishi wote na kuwapandisha madaraja yao

4. Taasisi za serikali na vyombo vya dola kama SUMA JKT, Magereza au NHC waache mara moja kupewa kazi bila kupitia ushindani. Tendering process

5. Ulipe madeni yote ya ndani. Hasa kwa supplies na contractors wote wanaodai serikali. Wengine zaidi ya miaka 5 wanadai

6. Ondoa Bashiru na Polepole hapa kwenye Chama

7. Focus kwenye maendeleo ya watu na sio vitu

8. Mpango asirudi wizara ya Fedha. Katupoteza sana hii miaka 5. Ndio maana njaa imetamalaki sana kwa wananchi na ndio tafsiri ya nyomi anayopata Lissu huko mkoani

9. Lazima ubadili baadhi ya sheria za sera kandamizi

10. Wale wasiojulikana washughulikiwe big time.

11. TRA ifumuliwe ili iwe mkusanyanyi friendly na sio kama wanavyofanya kazi sasa.

Tulivumilia hii miaka 5 tukaonekana wajinga. But katika hizi kampeni tumejaribu kutuma msg kupitia mikutano ya Lissu. Hivyo, basi tunaomba uyafanyie hayo kazi ili 2025 tuje tufanye kweli. Wewe ni mtu mwema sana ila ulizungukwa na viongozi wengine wa ajabu sana na ndio wamekuharibia. Like Mpango, Bashiru, Polepole na wale wengine kama Sabaya.
 
Wabongo mna vichwa vigumu!

Jiandae kwa hali ngumu zaidi iwapo atarudi madarakani kwani lazima ahakikishe miradi yake ya kipaumbele inakamilika kwani hana uhakika kama ataemrithi ataikamilisha. Sasa jiulize hali itakuwaje.

Itawachukua miaka mawili tu kuanza kujuta na kumkumbuka Lissu na aliyokuwa anayasema katika kampeni zake.

Ponepone yetu ni kumkataa tu kupitia sanduku la kura na kuhakikisha mshindi halali anatangazwa, vinginevyo tutajuta.

Time will tell.
 
Ni hivi, Magufuli hawezi kubadilika, hayo unayosema yamekwama kwa sababu yake na wala sio washauri wake. Msitake kuhamisha tatizo kwa hilo kundi la wapambe wanaomzunguka. Yeye ndio tatizo na hafai kuendelea kuwa raisi. Ww mpe lakini sisi wengine tuna maamuzi tayari, na tunataka box la kura liheshimiwe.
 
Kampeni za Lisu zimekushtua na zimeishutua CCM kuwa wananchi wengi hawakuridhika na namna ulivyoongoza katika kipindi hiki cha awamu ya kwanza.... Tumekaa na kufikiria tumeona tukupe kura as the last warning kwa CCM. Kama haya hayatafanyiwa kazi basi 2025 CCM isihangaike hata kuweka mgombea...
Mbona wenyewe wamekiri mkuu
 
Kampeni za Lisu zimekushtua na zimeishutua CCM kuwa wananchi wengi hawakuridhika na namna ulivyoongoza katika kipindi hiki cha awamu ya kwanza.... Tumekaa na kufikiria tumeona tukupe kura as the last warning kwa CCM. Kama haya hayatafanyiwa kazi basi 2025 CCM isihangaike hata kuweka mgombea...
Hawa kina Mpango, Bashiru, Polepole na hata Sabaya unawasingizia tu maana wanafanya kinachomfurahisha bosi wao.
 
Back
Top Bottom