Rais Magfuli, Msema kweli ni Mpenzi wa Mungu

Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
2,906
2,000
Niliwasikia Mbowe, Mbatia na Zitto wakitoa kauli kali kuhusiana na ajali ya MV Nyerere. Zitto anaendelea kutoa mawazo yake, ambayo ni mwiba kwa Utawala. Mbatia aliongea kama mtaalamu wa "majanga", na kwa kweli alikuwa "mpole" pale aliposema sasa siyo wakati wa "kulaumiana".

Mbowe alikuwa wazi zaidi katika msimamo wake.

ameshangaa muda mrefu uliopita kabla ya kazi ya uokoaji kuanza, wakati ajali imetokea mita 50 tu kutoka pwani. Yaani utadhania hiyo ilikuwa kafara ambayo imekusudiwa watu wengi wapoteze maisha, ili "sinema" ya uokoaji ianze. hakuna namna unaweza kueleza uchelewaji huu, na wala hakuna haja ya kumung'unya maneno hapa. Rais wetu ana tabia moja nzuri sana ya KUSEMA UKWELI, NA UKWELI DAIMA UNAUMA. PIA MSEMA UKWELI NI MPENZI WA MUNGU. Kama kuna mahali hiyo kauli inafaa kutumika, basi ni kwenye hili suala. Alichosema Mbowe ni ukweli mtupu ambao unahitaji kufanyiwa kazi kweli kweli. Mbowe pia alishangaa kwamba kazi ya uokoaji katika kile kipindi muhimu sana cha mwanzo, ilifanywa na wavuvi na wananchi wengine wa kawaida. hapakuwa na kikosi maalum cha waokoaji, wenye zana za uzamiaji.

Ingawa Rais Magufuli ametekeleza baadhi ya yale ambayo Mbowe alimtaka afanye, kwa mfano kufanya mazishi ya kitaifa, kuhutubia taifa, kutoa fidia kwa wafiwa, na mengine, kauli aliyotoa kwamba WANASIASA WASITUMIE VIFO VYA WATANZANIA KUTAFUTA KIKI ZA KISIASA, ilikuwa na lengo la kumpuuza Mbowe, na kuendeleza kile ambacho amekuwa akikifanya, kuondoa kabisa dhana ya upinzani, kuwapuuza wapinzani, na kuonesha kwamba serikali inatosha kabisa wala haihitaji chombo cha kuikosoa na kuishauri. Baada ya kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa, baada ya kubadilisha kabisa utaratibu wa uchaguzi, na kuwezesha vyombo mbalimbali vya serikali kuipa CCM ushindi wa asilimia 100 katika chaguzi zote ndogo. sheria zimewekwa kando, vyombo vinafanya chochote kinachowezekana alimradi ushindi uende kwa wagombea wa CCM. Kwa kauli yake, Rais Magufuli alilenga kuendeleza upuuzaji wa wanasiasa wa upinzani, kubeza lolote wanalosema. Kwa hili, Rais anahitaji kujifunza kuupokea UKWELI pale anapoambiwa.

Mbowe, Mbatia, Zitto, ni wakuu wa vyama vya siasa, ambavyo vina usajili wa kudumu, vipo kwa mujibu wa sheria. wanayofanya ni kwa mujibu wa sheria. kama wanakosea, sheria pia zipo za kuwahukumu.

Inaonekana Rais amesahau kwamba hana mamlaka ya kuwapangia wanasiasa waseme nini, alimradi hawavunji sheria za nchi. ni wazi kwamba tukio la ajali ya MV Nyerere limetuonesha wazi maeneo ambayo yana mapungufu makubwa katika nchi yetu. ukweli kwamba tayari nchi yetu imepatwa na ajali nyingi kubwa na ndogo, za vyombo vya majini, na bado hatuoneshi kuwa na utayari wa aina yoyote au hata tahadhari yoyote inachukuliwa kulinda maisha ya watanzania.

Lakini pia kuna ukweli mwingine:
1) Serikali inahimiza watu wachangie. michango hii iwe ni kwa ajili ya wahanga wa ajali hii. isiwe tena yakatokea yale yaliyotokea wakati wa Tetemeko la Bukoba. Serikali iliitisha michango, watu na taasisi mbalimbali wakaitikia. Serikali ya JPM ikashikwa na tamaa na kupora fedha zile na kudai kwamba ni kwa ajili ya miundombinu iliyoharibika Kagera. Hatungependa tabia hiyo ijirudie katika msiba huu wa MV Nyerere. Kama serikali inataka kuitisha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya miundombinu, iseme hivyo toka mwanzo. siyo tabia nzuri kujifanya unataka watu wachangie waathirika, kumbe unatumia vibaya huruma za watanzania kwa waathirika.

2) Hii tabia ya Rais wetu, ambaye licha ya kuwa ni COMMANDER IN CHIEF, lakini pia ndiye COMFORTER IN CHIEF, inaonekana Rais wetu ama hajitambui, ama kuna tatizo kubwa sana ambalo hatuambiwi. Iweje Rais wetu haonekani katika misiba mikubwa ya kitaifa? Tetemeko la Bukoba, Ajali ya Wanafunzi Arusha, na hii ya MV Nyerere? Lakini pia kuna tukio lile la wanajeshi wetu waliouwawa kule DRC Congo, siku ambayo wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, na taasisi nyingine kubwa, walimiminika hapa kwetu kuungana na sisi katika kupokea na kutoa heshima za kitaifa kwa miili ya askari wetu waliokufa vitani. Amiri Jeshi Mkuu wetu siku hiyo hakuwepo, bali alikuwa Dodoma anafungua tawi la Benki ya CRDB, ambalo hata Mkuu wa Mkoa ni mkubwa mno kwa kazi hiyo. hiyo ni labda Mkurugenzi wa Halmashauri alitosha kabisa kwa kazi hiyo. Lakini kazi ikafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ama kwa kutojua, ama kwa sababu yoyote ile, Ukweli ni kwamba hizo siyo tabia njema kwa mzalendo namba moja wa Taifa letu. HUO NDIO UKWELI NA UKWELI UNAUMA.
 
Fernando Jr

JF-Expert Member
Jul 12, 2017
1,953
2,000
Mheshimiwa akisoma hili bandiko akalielewa kabisa, naamini ataanza kubadilika japo taratibu. Ila akifungua na kuanza kusoma huku akiwa amekunja ndita, ataishia kukasirishwa na ukweli mchungu kwake uliojaa humu. Mwisho ataendelea kuharibu na kuharibikiwa zaidi hadi mwisho wa utawala wake.

Ushauri mdogo tu: Hakuna aliyefanikiwa bila kulaumiwa na/ama kukosolewa. Kusifiwa pekee hakusaidii kitu, kunafurahisha tu nafsi lakini mwisho wake ni mtaroni.

Hilo la kutokuhudhuria misiba limeanza sasa kunihamishia kwenye ulimwengu wa kiroho, si kawaida aisee.
 
pilipili kichaa

JF-Expert Member
Sep 3, 2013
10,630
2,000
Isaya 10: 1 - 4 'Ole wao wanaotunga sheria zisizo na haki, watu wanaopitisha sheria za kukandamiza. Je mtafanya nini siku ya adhabu, siku dhoruba itakapowajieni kutoka mbali? Mtamkimbilia nani kuomba msaada? Mtakwenda wapi kuweka mali yenu? Litakalowabakia ni kujikunyata kati ya wafungwa'
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
2,906
2,000
Mheshimiwa akisoma hili bandiko akalielewa kabisa, naamini ataanza kubadilika japo taratibu. Ila akifungua na kuanza kusoma huku akiwa amekunja ndita, ataishia kukasirishwa na ukweli mchungu kwake uliojaa humu. Mwisho ataendelea kuharibu na kuharibikiwa zaidi hadi mwisho wa utawala wake.

Ushauri mdogo tu: Hakuna aliyefanikiwa bila kulaumiwa na/ama kukosolewa. Kusifiwa pekee hakusaidii kitu, kunafurahisha tu nafsi lakini mwisho wake ni mtaroni.

Hilo la kutokuhudhuria misiba limeanza sasa kunihamishia kwenye ulimwengu wa kiroho, si kawaida aisee.
Na anayependa kusifiwa tu, ana matatizo ya kisaikolojia. Ni mgonjwa anahitaji ushauri nasaha. cha ajabu anaonekana shujaa. inaoenekana Tanzania wengi tu wagonjwa wa akili...
 
Eng Inc

JF-Expert Member
Feb 3, 2017
499
1,000
Na anayependa kusifiwa tu, ana matatizo ya kisaikolojia. Ni mgonjwa anahitaji ushauri nasaha. cha ajabu anaonekana shujaa. inaoenekana Tanzania wengi tu wagonjwa wa akili...
Ni kweli kabisa wengi watanzania sisi akili zetu hazipo sawa tukiongozwa na chama tawala
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
3,544
2,000
Prof Shivji kasema hakuna Kiki ya siasa kwenye misiba watu wachangie Kwa kulia, kw a upole,Kwa kukaripia nk.sasa mheshimiwa anataka atuzibe midomo
Wanaotafuta KIKI za kisiasa ni wale tunaowaona wamevalia mavazi ya chama chao Msibani. Mengine ni kujifaragua tu baada ya kutia aibu. Kila anayesimama msibani anasema fulani amehuzunika sana na anawapa pole. Utafikiri huyo fulani yuko Mbinguni kumbe anapata kifungua kinywa hapo jirani tu.
 
Abunwasi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
5,480
2,000
Niliwasikia Mbowe, Mbatia na Zitto wakitoa kauli kali kuhusiana na ajali ya MV Nyerere. Zitto anaendelea kutoa mawazo yake, ambayo ni mwiba kwa Utawala. Mbatia aliongea kama mtaalamu wa "majanga", na kwa kweli alikuwa "mpole" pale aliposema sasa siyo wakati wa "kulaumiana".

Mbowe alikuwa wazi zaidi katika msimamo wake.

ameshangaa muda mrefu uliopita kabla ya kazi ya uokoaji kuanza, wakati ajali imetokea mita 50 tu kutoka pwani. Yaani utadhania hiyo ilikuwa kafara ambayo imekusudiwa watu wengi wapoteze maisha, ili "sinema" ya uokoaji ianze. hakuna namna unaweza kueleza uchelewaji huu, na wala hakuna haja ya kumung'unya maneno hapa. Rais wetu ana tabia moja nzuri sana ya KUSEMA UKWELI, NA UKWELI DAIMA UNAUMA. PIA MSEMA UKWELI NI MPENZI WA MUNGU. Kama kuna mahali hiyo kauli inafaa kutumika, basi ni kwenye hili suala. Alichosema Mbowe ni ukweli mtupu ambao unahitaji kufanyiwa kazi kweli kweli. Mbowe pia alishangaa kwamba kazi ya uokoaji katika kile kipindi muhimu sana cha mwanzo, ilifanywa na wavuvi na wananchi wengine wa kawaida. hapakuwa na kikosi maalum cha waokoaji, wenye zana za uzamiaji.

Ingawa Rais Magufuli ametekeleza baadhi ya yale ambayo Mbowe alimtaka afanye, kwa mfano kufanya mazishi ya kitaifa, kuhutubia taifa, kutoa fidia kwa wafiwa, na mengine, kauli aliyotoa kwamba WANASIASA WASITUMIE VIFO VYA WATANZANIA KUTAFUTA KIKI ZA KISIASA, ilikuwa na lengo la kumpuuza Mbowe, na kuendeleza kile ambacho amekuwa akikifanya, kuondoa kabisa dhana ya upinzani, kuwapuuza wapinzani, na kuonesha kwamba serikali inatosha kabisa wala haihitaji chombo cha kuikosoa na kuishauri. Baada ya kupiga marufuku shughuli za vyama vya siasa, baada ya kubadilisha kabisa utaratibu wa uchaguzi, na kuwezesha vyombo mbalimbali vya serikali kuipa CCM ushindi wa asilimia 100 katika chaguzi zote ndogo. sheria zimewekwa kando, vyombo vinafanya chochote kinachowezekana alimradi ushindi uende kwa wagombea wa CCM. Kwa kauli yake, Rais Magufuli alilenga kuendeleza upuuzaji wa wanasiasa wa upinzani, kubeza lolote wanalosema. Kwa hili, Rais anahitaji kujifunza kuupokea UKWELI pale anapoambiwa.

Mbowe, Mbatia, Zitto, ni wakuu wa vyama vya siasa, ambavyo vina usajili wa kudumu, vipo kwa mujibu wa sheria. wanayofanya ni kwa mujibu wa sheria. kama wanakosea, sheria pia zipo za kuwahukumu.

Inaonekana Rais amesahau kwamba hana mamlaka ya kuwapangia wanasiasa waseme nini, alimradi hawavunji sheria za nchi. ni wazi kwamba tukio la ajali ya MV Nyerere limetuonesha wazi maeneo ambayo yana mapungufu makubwa katika nchi yetu. ukweli kwamba tayari nchi yetu imepatwa na ajali nyingi kubwa na ndogo, za vyombo vya majini, na bado hatuoneshi kuwa na utayari wa aina yoyote au hata tahadhari yoyote inachukuliwa kulinda maisha ya watanzania.

Lakini pia kuna ukweli mwingine:
1) Serikali inahimiza watu wachangie. michango hii iwe ni kwa ajili ya wahanga wa ajali hii. isiwe tena yakatokea yale yaliyotokea wakati wa Tetemeko la Bukoba. Serikali iliitisha michango, watu na taasisi mbalimbali wakaitikia. Serikali ya JPM ikashikwa na tamaa na kupora fedha zile na kudai kwamba ni kwa ajili ya miundombinu iliyoharibika Kagera. Hatungependa tabia hiyo ijirudie katika msiba huu wa MV Nyerere. Kama serikali inataka kuitisha harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya miundombinu, iseme hivyo toka mwanzo. siyo tabia nzuri kujifanya unataka watu wachangie waathirika, kumbe unatumia vibaya huruma za watanzania kwa waathirika.

2) Hii tabia ya Rais wetu, ambaye licha ya kuwa ni COMMANDER IN CHIEF, lakini pia ndiye COMFORTER IN CHIEF, inaonekana Rais wetu ama hajitambui, ama kuna tatizo kubwa sana ambalo hatuambiwi. Iweje Rais wetu haonekani katika misiba mikubwa ya kitaifa? Tetemeko la Bukoba, Ajali ya Wanafunzi Arusha, na hii ya MV Nyerere? Lakini pia kuna tukio lile la wanajeshi wetu waliouwawa kule DRC Congo, siku ambayo wawakilishi wa Umoja wa Mataifa, na taasisi nyingine kubwa, walimiminika hapa kwetu kuungana na sisi katika kupokea na kutoa heshima za kitaifa kwa miili ya askari wetu waliokufa vitani. Amiri Jeshi Mkuu wetu siku hiyo hakuwepo, bali alikuwa Dodoma anafungua tawi la Benki ya CRDB, ambalo hata Mkuu wa Mkoa ni mkubwa mno kwa kazi hiyo. hiyo ni labda Mkurugenzi wa Halmashauri alitosha kabisa kwa kazi hiyo. Lakini kazi ikafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Ama kwa kutojua, ama kwa sababu yoyote ile, Ukweli ni kwamba hizo siyo tabia njema kwa mzalendo namba moja wa Taifa letu. HUO NDIO UKWELI NA UKWELI UNAUMA.
Ni kweli kabisa kwani kila tundu ambalo mnaona hapa ndiyo mmempata mnakuja kugundua kwamba ndiyo mnazidi kumpaisha.
'A rose by any name remains just as sweet'
 
Mindi

JF-Expert Member
Apr 5, 2008
2,906
2,000
Ni kweli kabisa kwani kila tundu ambalo mnaona hapa ndiyo mmempata mnakuja kugundua kwamba ndiyo mnazidi kumpaisha.
'A rose by any name remains just as sweet'
aisifuye mvua imemnyea, walisema wahenga. huo "usweet" wa rose unaousikia kwa Magu, heri yako wewe. wengine wanasikia harufu ya mizoga iliyooza. waliobomolewa nyumba zao, walioondolewa kwenye ajira kwa kuhojiwa vyeti ambavyo hawakuhojiwa wakati wa ajira, walionyimwa malipo halali ya ongezeko la mshahara na kufutwa promosheni zao, na walala hoi wengi waliokosa ajira kwa sera za Magu, licha ya watanzania kwa ujumla wanaolia "kubana kwa vyuma". Magu anapaaje kwa mtu ambaye sasa anapata mlo mmoja kwa siku, tofauti na zamani?
 
Ni kweli kabisa inabidi waende kumuona otorhinolaryngologist
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom