RAIS Lowassa, Waziri Mkuu Chenge!!!!

Status
Not open for further replies.

Tina

JF-Expert Member
Jul 9, 2007
572
580
NIKIWA Dar, kabla sijagundua kwamba nilikua niko ndotoni, nilijikuta niko nchini Kenya, nikiwa mkimbizi niliyeponea chupuchupu baada ya wenzangu watatu kuuwawa na askari wa serikali yaliyovamia ofisi zetu katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Wakati huo, Rais Edo Lasaswa, alikua akikutana na Waziri Mkuu wake, Anda Changa la Macho, huku Waziri wa Fedha, Uchumi, Mipango na Biashara ya Nje, Rasta wa Mazizini, akiwa anakutana na Wafanyabiashara wa ndani katika Hoteli ya Kitalii ya Kampasua.

Wakati hayo yakiendelea, Waziri wa Usalama wa Raia, na Mambo Nyeti, Pitia Soro wa Ukambani, alitembelea ofisi zetu na kulaani vikali kitendo cha askari wake kuvamia ofisi zatu na kuunda tume itakayoongozwa na Jaji Mkuu Profesa Costume Mahela.

Ndoto yangu ilikatika katika…. Nikazinduka nikiwa natweta jasho likiwa linanitoka wakati usiku huo kulikua na mvua kubwa inanyesha… ndio maana sikutaka kuwasiliana na mtu hadi nimeamini nimeshaondoka Bongo….. mhnnnnn samahani sana kama nimewapa kisichostahili, lakini tokea nikiwa mdogo ndoto zangu zote mara nyingi huwa za kweli hata kama zinachelewa kudhihirika.


NATOA IDHINI KWA Mode kuiondoa mara moja ikiwakera watu. Sina kinyongo wenye kupenda waweke kumbukumbu tukiwa HAI
 
Tina fafanua ndoto yako inawezekana umenusa kitu au otherwise tumeshindwa kujua kama ni ndoto au ni nini ?
 
ndoto yako inatisha, sasa sijui ukae macho maisha yako yote hili usiote tena ndoto kama hii.

Mungu tubaliki Watanzania
 
Bongo yote yanawezekana,edo juzi kasafishwa,Rasta mazizi Igunga wamegoma asijing`atue ubunge,

Tina tuletee ndoto nyingine tafadhali !!!!!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom