Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Wiki iliyopita mitandaoni kulikuwa na clip ya video inayomuonyesha Rais Magufuli akifanya kikao na uongozi wa juu wa BOT, akiwepo pia waziri wa fedha. Mengi yaliongelewa kwenye kikao hicho lakini moja ambalo limenifanya niwaze kwa mapana ni hili la Rais kuagiza malipo ya zaidi ya shilingi bilioni 900 kwenda kwa wanaoidai serikali, yasitishwe kwanza, ili uhakiki wa kina uweze kufanyika, na fedha iende kwa taasisi ambayo kweli inaidai serikali.
Zaidi ya shilingi bilioni 900 ni fedha nyingi, na kwangu binafsi ni mara ya kwanza kumsikia rais wa nchi hii akitoa maagizo kama aliyoyatoa akiwa na mabosi wa BOT na waziri wa fedha. Kwenye malipo na manunuzi ndipo penye udhaifu mkubwa sana, na kashfa nyingi zinazoihusu BOT huwa na uhusiano na manunuzi pamoja na malipo.
Fedha ya nchi hii iliachwa mikononi mwa wachache, wakazungukwa na wanasiasa walafi, matokeo yake ndio hizo kashfa za wizi wa mabilioni ya fedha. Enzi za nyuma tusingeweza kumsikia rais akiongelea juu ya umuhimu wa kila senti kwenda kwa yule mwenye kustahili kulipwa. Watu walikuwa wakicheza na namba kadri iwezekanavyo, zero zilikuwa zikiongezwa kirahisi tu. Natumaini huu hautakuwa mwisho wa serikali ya awamu ya tano katika kuhakikisha kunakuwepo na ufuatiliaji wa karibu wa mzunguko wa fedha za serikali.