stigajemwa
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 449
- 430
Wanabodi;
Nianze kwa kukumbushia msimamo wa Rais wa JMT kuwa katiba mpya si kipaumbele chake. Lakini kwa namna mambo yanavyokwenda bado inambidi aikubali katiba pendekezwa ya Warioba.
Imekuwa ni kawaida sasa kusikia Rais kafanya uteuzi Fulani.Yaani toka ameingia madarakani ni miaka mitatu lakini bado hajamaliza kuunda serikali.
Hii inatokana na ubovu wa katiba tuliyonayo ambayo inampa mamlaka makubwa rais, mojawapo ikiwa ni hiyo ya kuhusika na teuzi zote za watendajia na viongozi wa serikali bila mipaka.
Hasara ya jambo hill ni Rais kuteua viongozi na watendaji wabovU hivyo kujikuta kila Siku anateua na kutumbua kwa sababu ikulu pekee haina uwezo wa kutambua sifa na tabia za kila RAIA anayefaa kuwa kiongozi au mtendaji ndani ya nchi kubwa kijiografia na idadi ya watu kama Tanzania
Katiba pendekezwa ya Warioba ilimwekea mipaka Rais ktk teuzi zake,ambapo ilipendekeza kuwepo kwa kamati zinazohusika na kuandaa orodha ya wenye sifa husika kisha kupitia orodha hiyo ndio Rais anateua.
Katiba ya Warioba ingemsaidia rais kuokoa pesa za walipa kodi kwani hawa wanaotenguliwa kwa kukosea scouting wanarigharimu Taifa pesa nyingi.
Tumechoka hii hali Leo unateua mkurugenzi Takukuru kesho umemtengua,kesho kutwa mkurugenzi halmashauri Fulani siku inayofuata umemtengua.
Hawa wote wanaotenguliwa hulazimika kulipwa kwa kuwa utenguzi wao huwa ni mabadiliko ya kawaida ya kiutendaji. Au hulazimika kubadilishiwa kazi hivyo kuwa mzigo kwa Taifa.
Taifa linahitaji mfumo maalum unaohusika na scouting, mfumo ambao unahusisha kamati ya wataalamu wa fani husika ambao wanafanya kazi ya kuandaa orodha ndefu ya wadau wenye sifa. Kazi ya Rais inakuwa ni kupitia orodha hiyo na kufanya uteuzi.
Hii itaondoa kuwa na wateule wenye sifa zinazotia shaka kimaadili na kiutendaji kama ilivyo sasa kwa teuzi nyingi za wakurugenzi wa mashirika ya umma,wakurugenzi halmashauri mbalimbali, wakuu wa Wilaya na mikoa.
Miaka mitano itakwisha Rais anafikiria kuteua na kutengua badala ya kufikiria kuboresha maisha ya Watanzania.
Nawasilisha.