Elections 2010 rais kwa 61.17%?

kachumbari

Senior Member
Nov 1, 2010
125
8
Kaka inabidi ujitahidi urudishe imani kwa walio kuajiri.
Lazima ufanye OVERTIME! la sivyo..........! miaka 5 ijayo, Chama kubwa Bye! bye!.
 
Kikwete amechagulwa kwa 27% ya wapiga kura wote walioandikishwa, waliopiga kura ni 41% pekee, sehemu kubwa ya 59% ni wale walioamini uchaguzi utachakachuliwa tuu, kazi iliyopo mbele yetu wana CHADEMA ni kuhakikisha tunarudisha matumaini kwa watanzania wasiotaka kupiga kura ili tukijumlisha na 26% ya Dr Slaa tutapata ushindi wa kimbunga 2015
 
Umesema kweli. Naomba Chadema waitishe mkutano wa wapenzi wao nchi nzima katika harakati za kukijenga chama. Waimalishe mtandao wa chama ili 2014 washiriki kikamilifu serikali za mitaa kujiandaa kwa ushindi 2015
 
Twende mbele turudi nyuma, wengi wetu humu JF tujitokeze tukagombee, Akina Slaa wametimiza wajibu wao, tuwaunge mkono, record ya kura inaonesha kuwa sehemu ambazo chadema iliweka mgombea mwenye nguvu, elimu na uwezo wa kujenga hoja wa udiwani na ubunge Slaa amepata kura za kutosha lakini ameangushwa na wagombea wabovu.

vijana tujitokeze tukafanye kampeni na kuomba kuchaguliwa ili tusaidie harakati, ndiyo maana mimi nimeamua kujitokeza kugombea Isimani Iringa uchaguzi ujao na naanza maandalizi mara moja

Mfano halisi ni Tundu Lisu ambaye ameshinda singida kwa mara ya kwanza upinzani kupata jimbo kule, wakati tundu kashinda singida kusini singida kaskazini mgombea wa sisiem kapata 90% maana yeke ni kwamba wananchi wanaelewa na wanajua kuchambua pumba na mchele

lazima tuanzisha movement sasa ya kupata wagombea sahihi kila jimbo nchi nzima 2015
 
Kikwete kashindwa uchaguzi For the second term president kushindwa kufikia hata asilimia ya uchaguzi wa mwanzo ni aibu
 
Waliopiga kura Milioni 8+
Kikwete kapata asilimia 61.1 ya hizo kura mil 8+
Dr. Slaa kapata asilimia 26.

Waliojiandikisha ni watu milioni 16.6 bila kujumlisha idadi ya Kiravu ya watu mil. 3.
Hivyo kumbe watu wote wangepiga kura SLAA angenyakua Asilimia 79, JK 18, na Lipumba 2, Asilimia moja iliyobaki wangenyang'anyana akina Rungwe.
 
Twende mbele turudi nyuma, wengi wetu humu JF tujitokeze tukagombee, Akina Slaa wametimiza wajibu wao, tuwaunge mkono, record ya kura inaonesha kuwa sehemu ambazo chadema iliweka mgombea mwenye nguvu, elimu na uwezo wa kujenga hoja wa udiwani na ubunge Slaa amepata kura za kutosha lakini ameangushwa na wagombea wabovu.

vijana tujitokeze tukafanye kampeni na kuomba kuchaguliwa ili tusaidie harakati, ndiyo maana mimi nimeamua kujitokeza kugombea Isimani Iringa uchaguzi ujao na naanza maandalizi mara moja

Mfano halisi ni Tundu Lisu ambaye ameshinda singida kwa mara ya kwanza upinzani kupata jimbo kule, wakati tundu kashinda singida kusini singida kaskazini mgombea wa sisiem kapata 90% maana yeke ni kwamba wananchi wanaelewa na wanajua kuchambua pumba na mchele

lazima tuanzisha movement sasa ya kupata wagombea sahihi kila jimbo nchi nzima 2015

Hapa point taken. Mimi nimeanza maandalizi ya kwenda Njombe Magharibi na nilitangaza nia usiku ule nilipopata habari ya kuanguka vibaya kwa Mh. Nyimbo. Vijana tuna wezan lakini maandalizi ya mapema ni muhimu sana
 
Nilikuwa natafakari Jimbo la kugombea, tayari nimeamua kati ya majimbo mawili ya mkoa wa manyara. Babati Mjini, Au Hanang.
 
Binafsi, nasema hapana hadi hapo tutakapokuwa na KATIBA MPYA na TUME HURU YA UCHAGUZI. Katika mazingira ya sasa yaliyotumiwa na CCM kushinda uchaguzi huu, hakuna matarajio yoyote yenye matumaini kwa Upinzani huko tuendako. Upinzani unakuwa usindikizaji tu na hili linaniuma sana.

Niko tayari kwa harakati zozote zile zitakazopelekea kuundwa kwa katiba mpya itakayotoa Tume huru ya uchaguzi inayostahili kuitwa ya TAIFA. Kwa ufupi nimekata tamaa vibaya mno!
 
2015 itakuwa balaa maana kila chama kimeona mapungufu yake na kina kazi ya kujijenga ili kuhakikisha 2015 ni mpambano mkali kushika dola, sijui kutakuwaje na nani ataibuka mshindi maana hata CCM watakuwa na mgombea mpya
 
Na mimi najiandaa kugombea Jimbo la Buyungu ili tuikomboe kigoma kwenye makucha ya mnyonyaji ccm kwa asilimia 100
 
Back
Top Bottom