Waziri Ummy Mwalimu asema Wizara haina pesa kuwalipa Madaktari walioagizwa wawaajiri

Giltami

JF-Expert Member
Feb 23, 2017
892
1,232
Ifike hatue tuelewe kwamba huyu mtu hafai kuongoza.Waziri kasema wizara haina hela za kuwalipa watumishi ila watalipwa na rais hili sio jambo lá kufurahia anachounda rais ni kujipatia sifa yy tu.Atawalipa kwa mfumo upi au kwa mshahara wake?Kama hili likifumbiwa macho huenda vijana wanaohitimu wakanyanyasika ktk nchi yao.
IMG_20170420_070524_557.JPG
 
Waziri wa Afya, Jinsia, Wazee na Watoto jana alitoa taarifa kuwa Rais Magufuli ameagiza madaktari 258 waliokuwa wamekidhi vigezo vya kwenda kufanyakazi nchini Kenya waajiriwe na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania baada ya Mahakama Kuu ya Kenya kuweza zuio la muda kwa madaktari kutoka nje.

Jambo hilo lilipokelewa kwa furaha sana na watu wengi hasa wizara ya afya pamoja na Chama cha Madakatari, lakini sintofahamu kubwa iliyobakia ni, wapi zitakapopatikana fedha za kuwalipa wahudumu hawa wa afya ambao wataajiriwa serikalini.

Waziri Ummy Mwalimu alisema jana kuwa, kwa muda mrefu serikali ilishindwa kuajiri madaktari licha ya kuwa na uhaba mkubwa kutokana na kutokuwa na fedha za kuwalipa na kwamba hata hawa 258 watakaowaajiri yeye hajui fedha za kuwalipa zitatoka wapi. Ummy Mwalimu alisema yeye alipokea maagizo kutoka kwa Rais na hivyo Rais Magufuli ndiye anajua.

Jambo hili lilizua mvutano mkubwa miongoni mwa wachangiaji kwenye mitandao ya kijamii, wengi wakihoji ni wapi Rais anapopata fedha za kuajiri madaktari wakati wizara haina. Wachangiaji wengine walihoji ni mfumo gani unaotumika kuajiri watumishi kwa sasa serikali, kwa sababu inaonekana kama kila kitu ni hadi Rais Magufuli atakaposema.

Kuhusu ajira hizo, Waziri Ummy Mwalimu alisema kuwa majina ya madaktari hao ambao wameonekana ni wazalendo na kuwa licha ya vitisho vilivyokuwa vimetolewa kuhusu kwenda kufanya kazi Kenya lakini wao wakaomba, yatachapishwa kwenye tovuti ya wizara pamoja na wataalamu wengine 11.

Ajira hizo zitakuwa ni za kudumu na zitakuwa chini ya Wizara ya Afya, alisema Naibu Waziri Dr. Hamis Kigwangalla.

Swahilitimes
 
yani hawa wajinga huwa wananiudhi!!! Wangejua tunaivoisoma hiyo medicine wasingekua wanaongea ujinga ujinga hiivii!!! Basi kama ndio hivo waitoe au waisimanishe medicine kwa muda.... vichwa maji ao wasee****!!! yani wanaudhi sana mkuu.... despite of them to find out a solution or to remove root of the problem or to find alternative by arthmetic reasoning wenyewe wanafanya poor arthmetic calculation kama hayo maamuzi waliyotoa!! washaniaharibia siku hawa
 
Hana lolote ukweli lazima usemwe..huu ni ukurupukaji tuze maximum..nchi haiendeshi namna hiyo..suala la ajira idaya ya afya sio jambo la kuamka na kulitolea maamuzi mtu mmoja..
 
TUMBUA HUYU HAO WAFANYAKAZI 13000 HEWA PESA ZAO ZINAKWENDA WAPI SI WALIPE HAWA? HATA KAMA WALIKUWA WANALIPWA KIMA CHA CHINI CHA 250000 MARA 13000 ZINTOSHA HAO MADAKTARI WANAOLIPWA SIO ZAIDI YA 1200000 KWA MWEZI. si ziko kwenya bajeti inayisha juni mwaka hu? UTUONEE HURUMA SISI WALALAHOI HAO NDIO TUMAINI LETU KWA MATIBABU
 
Back
Top Bottom