Rais kuteua wapinzani baada ya wana CCM kushindwa kumsaidia

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
539
3,507
Nchi inahitaji mawazo chanya zaidi kuiongoza kuliko uungaji mkono wa kila kitu.Nchi inahitaji watu wabunifu na wenye mawazo yakutatua changamoto kuliko watu wasiotambua umuhimu wa nafasi zao na wanafiki.

Hii ni sababu mojawapo inayomfanya mhe Rais kuwaza kutafakari kuteua vijana na viongoz kutoka upinzani watakaomsaidia kuifikia Tanzania tuipendayo.

Ni mwito wangu kwa wale watakaoteuliwa kwenda kuonyesha utofauti na kuwafanya waliowengi kujitambua na kufanya kazi kwa ueledi ikiwa ni pamoja na kuwatatulia wananchi shida zao.

Ukiwa na viongoz wepesi kuandaa pongezi lakini si wepesi wakubuni mikakati ya kuwakomboa anaowaongoza Basi huyu siyo kiongoz Bali ni mchumia tumbo na ndio maana wakitumbuliwa wanakosa mwelekeo.Mhe. Magufuli amefika hapa alipo si kwa sababu ya kujipendekeza Bali ni kwakuchapa kazi na kuleta mabadiliko ya kweli toka akiwa Naibu waziri Hadi waziri na baadaye Rais.

Ni bahati mbaya Sana kwamba vijana na wateule wake wameshindwa kumuenzi kwa vitendo kwa kutatua changamoto badaya yake wamekuwa watu wa kuandamana. Angalia maandamano ya Jana Mtwara, angalia vikao vya RC Leo Arusha, angalia comments za bijana wa uvcc Leo utagundua wazi kwamba Hawa watu wanamkwamisha Mhe Rais na hivyo idea ya kuchukua watu wapya na kuwapa majukumu ndio kete itakayorudisha nidham ndan ya chama na kuwafanya watu wafanye kazi kwa ueledi na ubunifu.

Maendeleo hayana chama na tumeamua kufanya maendeleo shirikishi..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom