Rais kuteua makada UVCCM kuwa Wakurugenzi ni kuvuruga Utumishi wa Umma

Kwanza kwa nini DED awe ccm??? Hawa wanatakiwa kuwa Watumishi wa serikali!! Uzoefu wa kutosha unatakiwa mpaka mtu iwe Mkurugenzi. Kama Mkuu alitaka wajifunze basi angewaweka maassistants!

Ila hii tabia ya kutuambia kuwa mfanyakazi wa serikali asiwe na chama na hapo hapo unawanyima promotion kwa kuleta makada wa ccm kuwapa nafasi ambazo wao walistahili, na watakaofundishwa na hawa walionyimwa promotion to those positions ni kuwadhalilisha hawa senior staff na kuua kabisa motivation yao ya Kazi!!
Nakubaliana nawe Mkuu. Nadhani siku hizi huko Serikalini hakuna promotion, kwa kweli inawakatisha tamaa na kuwavunja moyo maafisa ambao walikuwa wawe promoted. Vitu vidogo vidogo kama hivi ndivyo vinavyo sababisha makosa haya tunayoshududia leo katika nyanja ya Utumishi na Utawala Bora. YAREKIBISHENI - HAYAPENDEZI.
 
View attachment 1877625
View attachment 1877629
View attachment 1877630

Hawa ni baadhi ya vijana wadogo kabisa toka UVCCM walioteuliwa kuwa makurugenzi.

KWA MUJIBU WA MEMORANDA YA FEDHA SERIKALI ZA MITAA(LGA) HAYA NDIO MAJUMKUMU MAZITO YA DED

1. Ensuring the existence of a formal and satisfactory system of financial administration;

2. Securing compliance with the prescribed financial procedures by operating departments;

3. Directing the work of the Internal Audit section, receiving their reports and after consultation with relevant head of departments, ensuring recommendations and acted upon and submitted to relevant authorities;

4. Overall management of Council’s expenditures, revenues, and all assets and liabilities;

5. Ensuring compliance of all statutory guidelines for the financial Management of Council affairs;

6. Responding to queries within given deadlines from the Office of the Controller and Auditor General, the Local Authority Account Committee (LAAC) and the Minister;

7. Making certain that councillors are kept regularly informed of the financial affairs of the Council;

8. Being secretary to the finance Committee;

9. Making sure that computerized system operates;

10. Keeping under good Custody all assets and property of the Council; and

11. Adhering to procurement functions stipulated in Public Procurement Act and its related

KWA TAFSIRI ISIYO RASMI

1. Kuhakikisha kunakuwa na mfumo rasmi na wakuridhisha katika usimamizi wa fedha

2. Kuhakikisha idara zinafanya matumizi kwa mujibu wa taratibu za fedha

3. Kuhakikisha kitengo cha ukaguzi wa ndani kinafanya kazi vyema, kupokea taarifa za ukaguzi wa ndani, na kwa kushirikiana na wakuu wa idara ahakikishe maoni ya mkaguzi wa ndani yanajibiwa na kutekelezwa na anawasilisha majibu hayo kwa mamlaka husika ambazo ni CAG, RAS na Chief Internal Auditor

4. Usimamizi wa matumizi, mapato, mali na madeni yote ya halmashauri kwa ujumla

5. Kuhakikisha sharia, sera, kanuni na miongozo yote ya usimamizi wa fedha za halamashauri inafuatwa.

6. Kuhakikisha kuwa anajibu kwa wakati hoja za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) na wizara

7. Kuhakikisha waheshimiwa madiwani wanapata taarifa za fedha za halamashauri

8. Kuwa katibu wa Kamati ya fedha ya Halamshauri. Kamati hii wajumbe wake ni madiwani.

9. Kuhakikisha mifumo ya kompyuta inafanya kazi

10. Kuhakikisha utunzaji mzuri wa mali za Halmashauri

11. Kuhakisha sharia ya manunuzi ya umma na kanuni zake zinafuatwa

MAJUMKU MENGINEYO

1. Kuidhinisha malipo

2. Kuidhinisha mikataba yote ya halmashauri

3. Kuteua Bodi ya Zabuni kwa mujibu wa sharia

4. Kuteua Kamati ya Ukaguzi(Audit Committee) kwa mujibu wa sharia

5. Kuwa mkurugenzi wa uchaguzi ngazi ya wilaya pale inapotokea

6. Kuteua kamati ya upembuzi wakati wa manunuzi makubwa

MY TAKE

Hii kazi sio rahisi kama mashabiki wa mwendo kasi mnavyodhani. Huyu mtu anaenda kuwa msimamizi wa idara 19 pale halmashauri. Ikiwepo idara ya elimu na afya zenye changamoto za kufa mtu. Huyu mtu ndio anaenda kukuza uchumi wa wilaya na kuongeza pato la taifa kupitia wilaya yake. Mikataba mikubwa ya mabilioni ya fedha za ujenzi wa miradi ya maendeleo inaenda kuidhinishwa na yeye baada ya kujiridhisha kila kitu kiko sawa.

Anakwenda kusimamia matumizi ya mapato ya ndani ya zaidi ya bilioni 20 mfano Manispaa ya Kinondoni mpaka milioni 500 kwa halmashauri mpya. Anakwenda kusimamia ruzuku ya serikali mabilioni ya fedha.

Anakwenda kusimamia ufungaji wa hesabu na kujibu hoja ngumu za CAG kama tulivyoona hapo juu, matokeo yake unashindwa kuzuia au kujibu hoja unaanda maburungutu ya kuhonga wakaguzi

Kwa maoni yangu, serikali isione aibu, pangia hawa watu wasio na sifa majuku mengine mara moja. System inajua nani mwenye uwezo na asiye na uwezo

Mjadala
Je, huku ni kunajisi utumishi wa umma?

Thanks
Haya yote ni mandalizi ya uchaguzi mkuu 2025.
 
Back
Top Bottom