Rais kuteua ma-Vice chancellor vyuoni; Katiba mpya itamke vipi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rais kuteua ma-Vice chancellor vyuoni; Katiba mpya itamke vipi?

Discussion in 'KATIBA Mpya' started by MNYISANZU, Dec 29, 2011.

 1. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #1
  Dec 29, 2011
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Huu ni mjadala, tujadili katiba mpya itamke vipi kuhusu hili?
   
 2. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #2
  Dec 29, 2011
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni suala la madaraka makubwa ya Rais haipaswi kuwa hivyo.
   
 3. Sooth

  Sooth JF-Expert Member

  #3
  Dec 29, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 3,773
  Likes Received: 4,496
  Trophy Points: 280
  Siasa ziwekwe mbali na maeneo ya kitaaluma. Kwa VC kuteuliwa na Rais, huko ni kuleta siasa vyuoni-kitu ambacho wote (bila kujali itikadi zetu) tutakuja kukijutia. Siku hizi hawa ma-VC hawafanyi tena kazi za taaluma, wao ni siasa mwanzo mwisho. Mfumo wa sasa haufai ktk mazingira haya ya siasa za vyama vingi na ushindani mkali wa sasa.

  Kila wanachokiamua, kwanza wanakuwa wamekiangalia kwa lenzi ya siasa. Mfano mzuri ni kufukuzwa wanafunzi UDSM hivi karibuni. Hawakuishia kuwafukuza tu, wameamua wasisome chuo chochote cha Umma na hata kupata mkopo wa bodi. Sasa hapa tujiulize UDSM wamepata wapi mamlaka ya kuzuia wanafunzi waliowafukuza wasidahiliwe vyuo vingine vya umma? Toka lini UDSM ikawa na mamlaka ya kuviamulia vyuo vingine vya umma kama sio siasa hizi?

  Mwisho nipendekeze mchakato wa kumpata VC uanzie ngazi za chini kabisa ktk chuo husika. Wahadhiri wapendekeze majina ambayo TCU watachagua mmojawapo. Hii itawafanya ma-VC kuwajibika kwa wanataaluma wenzao, badala ya kuwajibika kwa wanasiasa na chama tawala na kuwadharau wanataaluma wenzao kana kwamba hawajawahi kuwa wanataaluma.
   
 4. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,436
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  Nchi ya vilaza ..ndio tripolitania yetu hii
   
 5. OTIS

  OTIS JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 7, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Unatakaje? wapigiwe kura?
  Uchaguzi wa serikali ya wanafunzi uambatane na uchaguzi wa VC
  OTIS
   
 6. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #6
  Dec 29, 2011
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  Wasiwepo maana mi sioni kazi yao.
   
 7. m

  mpunze Member

  #7
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 20, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  inapaswa kuwa vipi?
   
 8. Chakunyuma

  Chakunyuma JF-Expert Member

  #8
  Apr 10, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 811
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kila chuo Kuna seneti(kikao cha directors and deans of faculties) hiki kikao ndio kichague kwa kupiga VC based on stated qualifications. Kwahiyo ni lazima mtu atimize vigezo Kabla ya kupigiwa kura.
   
Loading...