Rais kushindwa kutumia gari la wazi leo Dodoma ni ishara kuwa hatuko salama au ametishwa?

Benson Mramba

JF-Expert Member
Oct 29, 2013
644
1,482
Katika maisha yangu ndani ya siasa hasa wakati nikiwa mtumishi wa makao makuu ya Chadema tena niliyeaminika kuwa simuungi mkono Mwenyekiti bali ni kijana wa Zitto, nilijifunza kuwa hakuna watu wanaokuza mambo kama Walinzi wa viongozi wakati huo (Redbrigade)

Walinzi wanapenda kumuweka kiongozi mkuu katika hali ya hofu kubwa ili wapate kazi ya kufanya. Kipindi kile utasikia "mwenyekiti CCM wameandaa kama vijana mia tatu hivi so tunahitaji fungu la kazi maalum kuwafuatilia n.k ". Ukija kwenye vikao utasikia "Mwenyekiti mambo ya ulinzi ni very sensitive hatuwezi kuyaongea hapa hata bajeti yetu hatuwezi kuiwasilisha hapa tutakufuata tukupe details ila hali ni mbaya sana tunawindwa sana na hata humu ndani hatuko salama kuna watu humu sio wenzetu". Ukishasikia hivyo ujue wakienda kumuona huko faragha wewe unayeonekana kuwahoji na kuwapinga wanakubebesha usaliti kwa Mwenyekiti na kwasababu ya hofu wanayompa na wanavyomlinda asikutane na mtu mwingine ujue atawaamini tu na kuwaidhinishia fedha wanazotaka.

Sisemi vyombo vyetu vya ulinzi na usalama havina uadilifu kama hawa niliowaona hapana ila reporting ya walinzi huwa inatia hofu sana viongozi labda ni kwasababu ya uzito wanaoutoa kila wanapoona dalili za tishio.

Tangu Rais Magufuli aingie madarakani nimekuwa nikishuhudia ulinzi wa hali ya juu sana kiasi kwamba hadi unanikera mimi binafsi kama mshabiki wake. Sioni kwanini wamzongezonge Rais kiasi hicho wakati anawapenzi na mashabiki wengi sana huenda kuliko watangulizi wake kwa mtazamo wangu. Ndipo huwa napata mashaka kuwa wanataka kumtia hofu bure hasa ikizingatiwa amechukua hatua ngumu kwenye baadhi ya mambo.

Hili la leo ndio limenikwaza zaidi kiasi kwamba nahisi kuna siku Rais hatahudhuria matukio muhimu kwasababu tutakazoambiwa ni za kiusalama. Na je mbona Rais na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kila siku wanasema tuko SALAMA ila linapokuja swala la Rais tunaona vinginevyo?

Mwenyekiti wangu Mbowe aligombanishwa na kila mtu mzuri kwake na hawa hawa walinzi kwa kumjengea hofu na vitisho vingi mpaka mwisho wa siku amebaki amezungukwa na WANAFIKI na Wasaka FURSA. Rais wangu nae napata wasiwasi nae anaweza kufikishwa huko kwa kisingizio tu kuwa ana MAADUI wengi.

Mimi kama mwananchi sipendi Rais anavyozongwazongwa na tukio la leo ndio sijalipenda kabisa naomba Rais nae asikubali kubanwa kiasi hiki wananchi tunakerekwa. Na siamini kama ana maadui wengi kiasi hicho. Mtaani anapendwa sana. Ajiachie tu afanye kazi zake kwa Uhuru.
 
mara zote viongozi wetu siku ya Muungano,hasa rais huwa wanazunguka uwanja kweny gar la wazi uku wakiwa na mkuu wa Majeshi uku wakipungia mkono wananchi tofauti na leo ambapo leo.

Raisi wetu amezunguka kweny gar iliyozibwa uku akiwa amekaa na kuwapungia mikono wananchi kitu kil8choibua maswali

Raisi wetu anaumwa miguu?

au ni offuuu dhidi ya amaandamano?au waandamanji?
 
Raisi Magufuli hata akiamua kutembea kwa miguu saa sita ya usiku hakuna mtu atakaye mdhuru kwa sababu ni raisi anayependwa sana na wanyonge.
Mkuu uwezo wako wa kufikiri ni mdogo kuliko wa bata.

Kama anapendwa sana na wanyonge,je Tanzania yote wanaishi wanyonge pekee? Hao ambao mnaamini ni mafisadi nao ni wanyonge wanaompenda rais?

Mnabwatukaga tu ili muonekane mmesifia bila kufikiria.
 
Back
Top Bottom