Rais kupora hati ya kusafiria ya nyapara wa mafundi (Supervisor)

Pozzers

JF-Expert Member
Sep 14, 2013
337
560
Kitendo cha Rais kupora hati ya kusafiria ya nyapara wa mafundi (supervisor) raia wa India anaesimamia mafundi bomba wenzie kwenye mradi wa maji uko kusini mwa Tanzania ni kitendo kigeni kwenye ofisi za maRais Duniani:

Sio tu kwamba ni kitendo ambacho kina madhara makubwa kidiplomasia, lakini hakiongezi tija yoyote ya kimkataba na utekelezaji wa mradi huo. Fundi bomba wa kawaida hawezipata motisha au shinikizo kwakua makaratasi yake ya kupitia uwanja wa ndege yameporwa, badala yake fundi yoyote timamu angejisikia kubanwa na angepata msukumo kama angepata amri ya mahakama inayotoa sharti kwamba vifaa vyake (au mitambo yake) au account zake zitafungiwa kama atakua hajamaliza maradi kwa mujibu wa muda wa mkataba (sio muda wa rais); hiyo itakua ni baada ya kampuni ya fundi huyo imepata haki ya kusikilizwa (kwamba kwanini wamechelewa kumaliza mradi). Kama muathirika huyo wa matendo mageni ya ofisi za maRais atakua na nia ya kutoroka nchini kabla au baada ya kumaliza mradi huo basi atapata ushauri kutoka kwa wajuzi wa sheria za kimaifa kwamba akienda ubalozi wa India pale Kinondoni Ada estate akamueleza kwamba passport yake iliporwa, Balozi wake hatokua na budi kumpatia hati nyingine ya kusafiria. (Sisemi Bwana Rajendra Kumar atumie njia hii) nnachosema ni kuwa washauri wa Rais wa masuala ya Sheria wamuelekeze njia sahihi ndugu Rais kutekeleza nia zake 'njema'. Katika hatua hiyo Rais pia alimwambia fundi Kumar kwamba atamuonesha na atashughulika nae (Alisema kwa kingereza I will deal with you...., I will show you...)
Sijui nyie wenzangu mlielewa nini! Lkn kauli hii pia ni ngeni kama tendo la hapo juu.
Mkuu wa nchi ana'ahidi kumuonesha fundi bomba (mwenyezi Mungu aepushilie mbali) laki ikitokea leo Bwana Kumar amepatwa na jambo lolote baya (ajari kwa mfano) wenzetu wa India watatuelewaje ikiwa Rais wetu mwema alisema atamuonesha.
 
Yaani miaka miwili bado mradi kukamilika sasa mnazungunzia mahakama na sheria???

Sheria zipi? Je ni ni akina mama wangapi na watoto Lindi wamekufa kwa kukosa maji?

Tumwogope Mungu!

Kwa hili raisi yuko sahihi!
 
Mtoa mada una familia??mke/watoto/baba /mama?? Tuanzie hapo kwanza then tunaweZa kuendelea.. Au ww nawe ni jasiri km Mh Lema,Lissu!!ukinijibu nitashukuru sn otherwise km unaishi dalesalama tafadhari fungasha kilicho chako urudi kojomije...

I wish i culd be moderator..oppps sorry
I wish i culd be IGP...ooopp sorry
I wish i culd be RC
 
Kama ile katuni ya Gado ,Ling'ombe lumeingia duka la vyombo vya udongo.
Kila anapogeuka anavunja kitu

[HASHTAG]#bullinachinashop[/HASHTAG]
 
Back
Top Bottom