Lord Diplock MR
JF-Expert Member
- Mar 16, 2015
- 1,393
- 3,237
Sasa siri imefichuka ya jinsi mambo yanavyokwenda ndani ya bunge na sasa ni wazi bunge lipo chini ya ikulu!
Wakiongea jana katika kongamano la vijana wa CHADEMA lililofanyika katika ukumbi wa African Dreams hotel mjini Dodoma, wabunge Peter Msigwa, John Heche, Cecilia Pareso na Mwita Waitara waliwaeleza vijana kuwa bunge la sasa halina meno na kwamba lipo chini ya ikulu,
"Magufuli anampigia simu Spika wa bunge na kumuamlisha nini cha kufanya" John Heche
Aidha kitendo cha bunge kutokurushwa live pia kinaonekana japo hakijaasisiwa na ikulu ila sasa kimepata baraka zote za ikulu na kwamba spika yupo njia panda hajui atafanya nikimnukuu Mchungaji Msigwa "Spika wa bunge mwoga, mnafiki..." Mchungaji Msigwa ameenda mbali zaidi na kusema wabunge wengi wa ccm ni wanafiki wa kutupwa kwani wamekuwa wakiwaeleza wabunge wa upinzani jinsi wasivyofurahishwa na jinsi mambo yanavyokwenda wakiwa nje ya bunge na kwenye vikao vya kamati lakini wakiwa wanachangia ndani ya bunge utawaona wakisifia tena, wakitolea mfano swala la kutorushwa live kwa bunge kuwa wabunge wengi wa ccm wamewaambia hawajaliafiki lakini hutawaona wakilipinga ndani ya bunge.
Hata hivyo wabunge hao wameapa kuwa kama wabunge wa ccm wataendelea na unafiki wao waache kunung'unika mbele ya wabunge wa upinzani kuwa hawaridhishwi na mambo yanavyokwenda katika bunge na utawala wa JPM na kama wataendelea wao watawataja hadharani wabunge hao wanafiki!