R.B
JF-Expert Member
- May 10, 2012
- 6,296
- 2,575
Samahani kwa kuwataka radhi,
Natambua umuhimu wa idara hizi nyeti ni ngumu kuzitenganisha, lakini hazikwepi lawama kwa kutotimiza wajibu wao.
Rais na makamu wa rais ni meneja na strategic thinker wa nchi hii. Wanatakiwa kila wakiamka wafikiri hii nchi wanaitoaje kwenye dimbi la umaskini. Either kwa kutumia wataalamu wa ndani na wa nje. Na ikizingatiwa matatizo ya dunia ni ukosefu wa ajira ila kwa vijana ambao ni 65%.
Ikizingatiwa awamu hii g5, ni nchi ya viwanda. Tulitegemea mashirika, vyuo vikuu na midahalo mbalimbali, Kigoda cha Mwalimu, vyuo ya uhandisi, machapisho na vipeperushi ya kujadili kupitia media kama ilivyokuwa kipindi cha katiba mpya na uchaguzi mkuu, mada kubwa ingekuwa ni kujadili viwanda na ni viwanda vipi vinahitajika nchi hii, either kwa kutumia tiger plan kama nchi za Asia, kila mkoa au kanda mahitaji ya viwanda yanatofautiana.
Cha kushangaza hakuna anayeratibu mambo hayo!
Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu: Ingetakiwa iwe inajibu kila shutuma inayohusu rais ili kumpunguzia rais kujibu mambo ambayo hayana maslahi mapana ya nchi. Mfano ya LHRC, Rais Magufuli katumia muda mwingi kujibu shirika hili. Swali; Je, BAKWATA wakija na hoja zao, TEC, UKAWA, Magazeti ya ndani ya nchi, Raisi atakuwa ni mtu wa kujibishana tu?
Safari za rais zinaratibiwa na Kurugenzi, mbona hatupati mrejesho? Kinachofanyika ni kurusha taarifa na sio kutoa maelezo.
Katibu mkuu Kiongozi: Huyu tumezoea ndio utaoa taarifa kuhusu mambo ya matumizi ya pesa zinazorejeshwa kama za Uhuru, Bunge, mashirika, wahisani na kuzitolea maelezo jinsi rais alivyoelekeza.
Msemaji mkuu wa serikali: (alikuwa Ambwene), alitakiwa kuwa anatolea maamuzi bomba la gesi, mkopo wa MCC. Lakini cha kushangaza kila media, wizara ndo wasemaji.
Mambo ya nchi za nje: Tunajua ni waziri wa mambo ya nchi za nje.
Hizi idara zimpe rais muda wa kufanya mambo ya msingi .