Rais kuingilia utendaji wa NHC si sahihi

Joss

JF-Expert Member
May 28, 2009
765
191
Nimesoma habari katika Tanzania Daima yenye kichwa cha habari" NHC yarudisha funguo za wazazi ccm" NHC yarejesha funguo za wazazi CCM katika habari hiyo inaelezwa kuwa Rais ameliambia shiraka hilo kutafuta njia mbadala ya kudai madeni badala ya sasa ambayo inaathiri sana wizara. Mi naona hii si safi hata kidogo. Ndio yale ya Magufuli alipoambiwa aangalie utu/uungwana badala ya sheria katika bomoa bomoa, kwa hali hii tutafika kweli?
 
Kuingiza double standard kwenye utendaji huo tayari ni kuangusha bidii mpya ambazo ziliasisiwa ili kuleta mageuzi ya utendaji wa shirika hilo la umma.Hakika kwa picha hii HATUTAFIKA.
 
Neno muhimu hapo ni kutafuta namna mbadala ya kukusanya madeni hayo ili kuleta tija na malengo yale yale.
 
Ooooops! haya mambo ya kutafuta njia mbadala kwa matatizo sugu ndio yanayokwamisha taifa hili, huyu jamaaa ki ukweli mimi aninishangaza sana maana hizo njia mbadala zake pia hazifanikiwi, alitafuta njia mbadala za kulipa pesa za EPA hadi leo hatujui ziko wapi, njia mbadala kwa tatizo la umeme sote tunajua sasa tuko wapi! Serikali inadaiwa hakuna cha njia mbadala walipe tu!
 
Hii inamaanisha kua utendaji wa nhc si sahihi, sasa angetoa njia mbadala badala ya statement za juu juu. Ndio maana watendaji wengine wamejinyamazia kimya wanakula kinachopita kwenye 18 zao. Wanajua wakifanya kazi kwa principals wataingiliwa. Magufuli ni mfano halisi.
 
Huo ndio udhaifu wa rais wetu hawezi kusimamia sheria anaweza tu kuwachekea wavunja sheria hasa inapotokea anawafahamu
 
Neno muhimu hapo ni kutafuta namna mbadala ya kukusanya madeni hayo ili kuleta tija na malengo yale yale.

Kwa nini anaedai deni hatafute njia mbadala ya kudai na sio mdaiwa kutafuta njia mbadala ya kuondoa deni baada ya kula hela ya pango.
approach ya Raisi ingekuwa kwamba hao wanaodai wampe maelezo kwa nini hasiwafukuze kazi kwa kuhujumu shirika la umma (NHC) kwa kutolipa kodi, au raisi anajua hela ya pango ilikotumika
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Neno muhimu hapo ni kutafuta namna mbadala ya kukusanya madeni hayo ili kuleta tija na malengo yale yale.

Njia mbadala ni ipi hiyo kama watu wanadaiwa yapata miaka 3 mpaka 4 hawajalipa HAKIKA KWENYE MITI HAKUNA WAJENZI,ila matumaini yapo tutapata kiongozi wa juu ambae yeye safu yake ya utendaji ni watu aina ya Nehemia Mchechu na wakina John Pombe Magufuri ambao wapo tayari kusimamia utawala wa sheria na sio kufundisha jamii kukwepa sheria.Tunako kwenda watendaji wengi wa Serikali na hatimae Umma utaanza kupuuza sheria halali na hatimae tumeanza kuona jinsi raia wanavyojichukulia sheria mikononi na mwisho wake viongozi na familia zao ndio watakao pima ubaya wa kulea matumizi mabaya ya kupuuza utawala wa sheria kwa kuwa umma umetunga sheria lakini aliyepaswa kusimia sheria na kuona haki inapatikana kesha amua kukaa pembeni na kuacha kanuni ya mbugani au msituni [Jungle's Law] kuendelea kutumika na sio utawala wa haki na sheria kwa faida ya walio wengi.
 
Si maamuzi ya ajabu na kushangaza kwa Rais wetu huyu! Amezowea tumemzowea pia... Raha iliyoje?
 
Jibu rahisi ni kwamba Serikali Haiwezi Kufanya Biashara. Uliza idara za serikali ambazo zimepanga nyumba za watu binafsi kama zinachelewesha kulipa kodi na pesa zinatoka kwenye mfuko mmoja - Consolidated Fund
 
  • Thanks
Reactions: Nzi
Nani ana ushahidi wa maneno ya Rais yaliyowekwa hapa. Maana mjadala huu haumtendei haki Rais kabisa na unatuzuia wengine kuchangia mjadala bila ushahidi wa maneno ya Rais, kama kuna mtu anao basi auweke hapa.
 
Ushahidi upi unaoutaka sasa fafanua kauli yako plz..............Kauli ishatoka hv Magazeti yote yenye habari za Rais yabebe na ushahidi? naona kama huna hoja......
 
Nilishasema kuwa hayp ndiyo madhars ya kuongozwa na rais mswahili. Anachotafuta yeye ni misifa tu. Mambo ya utawala wa sheria ni msamiati usio kichwani mwake kabisa. Shame on you mkwe re.
 
nimesoma habari katika tanzania daima yenye kichwa cha habari" nhc yarudisha funguo za wazazi ccm" nhc yarejesha funguo za wazazi ccm katika habari hiyo inaelezwa kuwa rais ameliambia shiraka hilo kutafuta njia mbadala ya kudai madeni badala ya sasa ambayo inaathiri sana wizara. Mi naona hii si safi hata kidogo. Ndio yale ya magufuli alipoambiwa aangalie utu/uungwana badala ya sheria katika bomoa bomoa, kwa hali hii tutafika kweli?

hatuwezi kufika, kwani separation of power hakuna. Mpaka tutakapopata katiba mpya inayodhibiti madaraka ya rais.

Kwani hizo office si kila mwaka wanaomba fedha za bajeti ya wizara? Kwa nini wasilipe?
 
Back
Top Bottom